Watu 42 wamepoteza maisha na wengine 82 kujeruhiwa baada ya
mvua ya upepo mkali mkoani Shinyanga.
Mvua hiyo ambayo ilinyesha kwa muda mfupi imewaacha watu
3,500 bila makazi katika kaya 350 huku nyumba zikifurika maji na baadhi
ya mifugo ikisombwa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw. Ali Nasoro Rufunga amesema
mvua hiyo ya mawe iliyoambatana na upepo mkali ilisababisha mafuruko katika
kata ya Mwakata kuezua nyumba na nyingine kuanguka.
Amesema mali mbalimbali zimeharibiwa vibaya ikiwemo mifugo
kuzolewa na maji na vyakula kwenye eneo lote lililokumbwa na mafuriko hayo.
Hali ya majeruhi ambao wamepelekwa katika hospitali
mbalimbali bado sio nzuri kwa baadhi ingawa wengine wanaendelea vizuri.
EmoticonEmoticon