MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MBEWE WILAYANI MBOZI AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE KALI NA WATU WASIOFAHAMIKA



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 04.03.2015.

·         MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MBEWE WILAYANI MBOZI AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE KALI NA WATU WASIOFAHAMIKA.


·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE KWA TUHUMA MBALIMBALI.




KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MBEWE WILAYANI MBOZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FERUZI JAGRAS (36) ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI MARA TANO NA SHINGONI MARA MOJA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE MTO MUYOVIZI ULIOPO WILAYANI MBOZI.

MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA KWENYE MTO HUO MNAMO TAREHE 03.03.2015 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SHOMORA, KATA YA MALANGALI, TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.

AIDHA INADAIWA KUWA, MAREHEMU ALIONDOKA NYUMBANI KWAKE TANGU TAREHE 26.02.2015 KWENDA MATEMBEZINI KUSIKOJULIKANA. WATUHUMIWA WAWILI WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI AMBAO NI 1. PADRI MWIWA (48) MKAZI WA MBEWE NA 2. PETER MWAMENGO (51) MKAZI WA LUKULULU.



TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA AITWAYE MAISHA CHRISTOPHER (46) AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA MBILI [02].

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.03.2015 MAJIRA YA SAA 14:01 MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA ENEO LA ILEMI, KATA YA ILEMI, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.


KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WOTE WAKAZI WA AIRPORT JIJINI MBEYA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NILE MWALYEMBELE (58) NA 2. OSWARD MWANGOMOLE (40) WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI  [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05].

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.03.2015 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA ENEO LA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

 

AIDHA KATIKA MSAKO WA TATU, MTU MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA AITWAYE GODLUCK JOSEPH (18) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA KETE 183 ZA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAM 915.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.03.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI] NA POMBE YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU AU KIKUNDI CHA WATU WANAOJIHUSISHA NA UINGIZAJI/USAMBAZAJI NA UUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


                                               Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »