TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 18.03.2015.
·
KIJANA MMOJA MKAZI WA ITIMBO WILAYANI RUNGWE
AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI BAADA YA KUTOKEA UGOMVI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA MKAZI WA SIMBALIVE WILAYANI CHUNYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI, POMBE KALI NA
VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
KIJANA MMOJA
MKAZI WA ITIMBO WILAYANI RUNGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HODAR JOHN (22) ALIUAWA
KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI NA MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA GILBERT MWASIMA NA KUFARIKI DUNIA MUDA
MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MISHENI ITETE KWA MATIBABU.
TUKIO HILO
LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA TAREHE
17.03.2015 HUKO KATIKA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI KILICHOPO KATIKA
KITONGOJI CHA ITIMBO, KIJIJI CHA ISALE, KATA YA LUTEBA, TARAFA YA BUSOKELO,
WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI
ULIOTOKANA NA ULEVI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA KUWEZESHA KUMPATA MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
TAARIFA YA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU
WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA KISEPE
ALPHONCE (28) MFANYABIASHARA NA
MKAZI WA KASUMULU-KYELA PAMOJA NA NSAJIGWA
MWAKALONGE (39) DEREVA NA MKAZI
WA KYELA WAKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] KUTOKA NCHINI MALAWI ZILIZOPIGWA
MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA DOUBLE
PUNCH KATONI 70, BOSS KATONI 18,
CHARGER KATONI 14 NA RIDDER KATONI 08.
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.03.2015
MAJIRA YA SAA 03:00 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI NA KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA
MBEYA. WATUHUMIWA WALIKAMATWA WAKIWA WANASAFIRISHA BIDHAA HIZO KWENYE GARI
LENYE NAMBA ZA USAJILI T.479 CJM TOYOTA IPSUM LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA
NSAJIGWA MWAKALONGE WAKITOKEA
KASUMULU KUELEKEA MBEYA MJINI.
KATIKA
MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE
MMOJA MKAZI WA SIMBALIVE WILAYANI CHUNYA AITWAYE ELIZA KISUNGA (33)
MFANYABIASHARA NA MKAZI WA SIMBALIVE AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA
NNE NA NUSU PAMOJA NA POMBE KALI [VIROBA] AINA YA RIDDER PAKETI 03 NA VIPODOZI AINA YA EPIDEMIC PAKETI 02.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.03.2015
MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA SIMBALIVE, KIJIJI CHA ITUMBA, KATA YA CHALANGWA, TARAFA YA
KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA BIDHAA HIZO,
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUJIHUSISHA NA UINGIZAJI, USAMBAZAJI NA UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA
MARUFUKU NCHINI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE YA MOSHI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon