Polisi wakitoa mwili wa Mtoto huyo katika nyumba ambayo amefia. |
Wakazi wa Eneo la Veta wakishuhudia tukio hilo. |
Nyumba iliyotumika kwa kumbaka Mtoto huyo. |
Mama Mlezi wa Mtoto aliyefanyiwa ukatili akilia kwa uchugu mara baada ya kupata taarifa. |
Na Emanuel
Madafa,Mbeya
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya
msingi Ruanda Nzovwe jijini Mbeya Elika Mkumbwa( 8)amekutwa maekufa katika
jumba bovu (pagale) eneo la Mtaa wa Ilomba Village.
Akizungumzia
tukio hilo Balozi wa mtaa huo Ndugu Ezekiel Mwakalundwa amesema kuwa
amepata taarifa za kupatikana kwa mwili wa mtoto huyo majira ya saa 1 na
nusu asubuhi kutoka kwa majirani waliokuwa karibu na eneo.
Amesema
baada ya kupata taarifa hizo aliongozana na majirani pamoja na baadhi ya ndugu
wa marehemu huyo hadi eneo la tukio ambako kitendo hicho cha kikatili
I,mefanyika na kukuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umelazwa ndani ya sinki
la kuogea ndani ya moja ya chumba kwenye pagale hilo huku ukiwa hauna nguo.
Amesema
mara baada ya kuupekua mwili huo waligundua kuwa mtoto huyo aliofanyiwa vitendo
vya kikatili kuwa alibakwa ambapo sehemu zake za siri zilikuwa zimeharibika
bibaya na tayari mwili wake ulianza kuharibika na kuanza kutoa harufu.
Amesema
mara baada ya kushuhudia tukio hilo alitoa taarifa katika kituo cha polisi kati
ambapo polisi walifika na kuchukua mwili wa marehemu huyo ma kupeleka katika
hospital ya rufaa kwa ajili ya kuafanyiwa uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.
Amesema
kutokana na mazingira yaliyonekana katika eneo hilo huenda binti huyo alibakwa
hadi kufa kwani sehemu zake za siri zilikuwa zimeharibika vibaya.
Kwa upande
wao majirani wanao ishi karibu na eneo hilo wamedai kuwa tukio la kuwawa kwa
mtoto huyo si tukio la kwanza kwani matukio ya aina hiyo yamewahi tokea
zaidi ya mara tatu yakihusisha kubwakwa kwa watoto wadogo.
Mmoja wa
majirani hao aliyejitambulisha kwa nina la Kristina Mwakalundwa amesema
tukio hilo ni la tatu kutokea ambapo kuna mapagara pamoja na miti ya
mianzi ambayo ndio imekuwa chanzo cha kufanyikakwa matuki hayo ya
ubakaji.
Amesema
chanzo kingine cha tukio hilo kunatokana na baadhi ya wananchi kupanda mahindi
pembezoni mwa makazi ya watu ahali ambayo imekuwa ikichangia kwa kiwango
kikubwa kutoa mianya ya wahalifu kufanya vitendo vya kinyama vinavyo
fanana na tukio hilo .
Kufuatia
tukio hilo ameitaka serikali pamoja na wakazi wa eneo hilo kuungana kwa pamoja
kuhakikisha wanapinga hatua ya baadhi ya watu kuendeleza shughuli za kilimo
pembezoni mwa makazi ya watu.
Akizungumzia
kwa masikitiko makubwa mama mlezi wa mto to huyo Ndugu Sala Mwandobo amesema
binti yake alitoweka nyumbani toka jana January 7 mwaka huu nakwamba aliaga
nyumbani kuwa anakwenda kufua nguo za shule eneo la chemchem ya maji mita
kadhaa toka nyumabni anako ishi mtoto huyo.
Akielezea
zaidi mama huyo amesema kuwa yeye alikuwa safari na kwamba alirudi jana
hiyohiyo ambapo mara baada ya kurudi nyumbani alimkuta binti huyo akiwa
na sare za shule majira ya saa 9 mchana baada ya kulejea kutoka shule
ambapo mtoto huyo alikunywa chai kisha kumuomba mama yake kuwa
anataka kwenda kufua nguo kwani zimeloa ambapo alimruhusu na kumtaka
awahi kurudi nyumbani .
Amesema
baada ya mtoto huyo kuondoka alichukua muda mrefu hali ambayo ilizua hofu
nyumbani kwako ambapo mama huyo aliagiza wenzankle kumfuata ikiwa majira ya saa
11 jioni ambapo hata hivyo hawakuweza kufanikiwa kumpata hivyo waliamua
kutoa taarifa kituo cha polisi ilomba majira ya saa 1 jioni .
Amesema
baada ya kutoa taarifa hizo kituo cha polisi waliendelea kutoa taarifa pia kwa
majirani huku wakiendelea kumtafuta hadi ilipo fika midaa ya saa6 usiku ambapo
walikata taamaa na kurudi nyumbani.
Amesema
ilipo fika asubuhi ya leo majira ya saa1 asubuhi walipata taarifa
za kukutwa kwa mtoto akiwa amekufa ndani ya pagale jirani na nyumbani kwao.
Amesema
baada ya kwenda kushuhudia mwili huo waligundua kuwa ni mtoto wake ambapo
alikutwa akiwa na ndoo pamoja na nguo alizokwenda kufua huku akidai kuwa
yawezekana watu hao waliofanya kitendo hicho walimkamatia maeneo hayo kabla ya
kufika eneo la kufulia nguo.
Amesema
inasikitisha sana na inamuuma sana kwani binti huyo alimchukua kwa mdogo wake
kijijini akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu akiwa katika hali mbaya ya kiafya
ambapo mapaka sasa umauti unamkuta mtoto huyo
Hata hivyo
kamanda wa polisi mkoa wa mbeya ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba mwili wa motto huyo umehifadhiwa katika hospital ya rufaa
mbeya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Mwisho.
Chanzo :faharinews.blogspot.com
EmoticonEmoticon