Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiendelea kutoa maelekezo ya Gari yake hiyo aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiwa na Meneja mkuu wa Alliance Autos Bwana Wayne Mcintosh(wa pili toka kulia)wakipata picha ya pamoja na wanahabari
Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed(kushoto)akipata picha na Dereva Rainer Zietlof
Meneja mkuu wa Alliance Autos Bwana Wayne Mcintosh akisoma cheti cha rekodi ya dunia alichopewa dereva toka ujerumani
DEREVA raia wa Ujerumani Rainer Zietlof yuko mbioni kuvunja rekodi ya dunia ya kuendesha gari kwa kilometa 17,000 kutoka Ulaya hadi Afrika.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Zietlof alisema kuwa hiyo
itakuwa ni rekodi yake ya tatu baada ya zile za awali alizovunja mwaka
2011 na 2012.
Awali
alivunja rekodi baada ya safari iliyojulikana kama 'Panamerica'ambayo
ilimchukua kutoka Tierra del Fuego hadi Alaska kwa siku 11 na saa 17
wakati ile ya 'Russtralia' ilimtoa Melbourne, Australia hadi
St.Petersburg nchini Urusi ambako alitumia saa 18.
Zietlof
anayetumia gari aina ya VW Touareg V6 TDI alianza rasmi safari yake
Septemba 21 mwaka huu huko North Cape nchini Norway na anatarajia
kuikamilisha nchini Afrika Kusini, ambako atakuwa ametembea kwa kilometa
17,000.
Kwa
mujibu wa dereva huyo, safari hiyo ndefu imempitisha katika nchi za
Norway, Finland, Sweden, Denmark, Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Slovakia,
Hungary, Serbia, Bulgaria, Uturuki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya na
sasa Tanzania.
Dereva
huyo alizungumza na wandishi wa habari katika makao makuu ya Alliance
Autos iliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa
atachangia kiasi cha senti 20 za euro kwa kila kilomita, kwa vijiji
nchini Tanzania na Zambia.
Mbali na kuahidi kuvichangia vijiji hivyo, Zietlot pia amesisitiza kuvitembelea vijiji hivyo atakavyo vichangia.
Aidha,
amelisifia gari hilo kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na mazingira
tofauti tofauti ya hali ya hewa kama baridi kali na joto pamoja na
barabara mbovu.
Mradi huu
wa kuzunguka sehemu mbalimbali za dunia kwa gari hilo umedhaminiwa na
makampuni makubwa ya magari ya Tehama na Volkswagen nchini Ujerumani,
Slovakia na Afrika Kusini.
Katika
safari hiyo Zietlow yuko na wasaidizi wake wawili, Marius Biela ambaye
ni mpiga picha na mchukua video huku Matthias Prillwitz ni mzoefu wa
mbio
za magari nchini Ujerumani.
Dereva huyo alianza safari zake za barabarani mwaka 2005 na ameoa na ana mtoto mmoja.
EmoticonEmoticon