GARI LA KAMPUNI YA MAGAZETI YA MWANANCHI LIMEKAMATWA NA POLISI.



GARI la kampuni ya Magazeti ya Mwananchi limekamatwa na Polisi mkoani Iringa kwa tuhuma ya yakusafirisha madawa ya kulevya aina ya Mirungi kutokea Dar kwenda Mbeya .
Taarifa za kiuchunguzi wa mtandao wa matukiodaima zimedai kuwa gari hilo limekuwa na kawaida ya kufanya biashara ya kufanya magendo kama ya vipodozi na mirungi kabla ya Polisi kuweka mtego jana usiku .
Hata hivyo mtego huo umefanikiwa kulikamata GARI hilo na magunia ya madawa hayo aina ya mirungi ambayo idadi yake bado kufahamika .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa amesema taarifa kamili ataitoa hapo baadae
  SOURCE :Matukio daima
Previous
Next Post »