
Rais Jakaya Kikwete akimpa cheti cha uraia wa Tanzania, Loveness Ruhaga
(kulia) aliyekuwa Mkimbizi kutoka nchini Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu
wa Tabora leo. Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156
na kuwatangazia kuwa sasa wamekuwa raia halali wa Tanzania hivyo wahakikishe
wanafuata sheria zote za nchi na waepuke kufanya vurugu za aina yoyote
kwani wakikiuka masharti hayo waweza kunyanganywa uraia huo. Wakimbizi
hao walioingia nchini tangu mwaka 1972 walionyesha furaha kwa kuimba
na kucheza vyimbo mbalimbali. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mathias Chikawe.

Msoma risala ambaye ni mwakilishi wa raia wapya 162,156 nchini ambao walikuwa wakimbizi kutoka nchini Burundi,
Dafroza Baragwimba akiisoma risala yao mbele ya Rais Jakaya Kikwete
(watatu kulia) wakati ya hafla ya utoaji wa vyeti kwa raia hao. Rais
Kikwete alitoa uraia kwa wakimbizi hao na kuwataka wawe waadilifu na
kufuata sheria zote za nchi. Wanne kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mathias Chikawe.

Rais Jakaya Kikwete akizungumza baada ya kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania, waliokuwa
wakimbizi 162,156 kutoka nchini Burundi walioingia nchini tangu mwaka
1972. Tukio la utoaji wa vyeti hivyo lilifanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora mjini humo leo. Raia Kikwete katika
hotuba yake aliwataka raia hao wapya kuwa waadilifu na kufuata sheria
zote za nchi. Wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe, wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil
na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke.

Sehemu ya wakimbizi wa Burundi 162,156 ambao sasa ni raia wa Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete
kuwapa uraia katika halfa iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo. Rais Kikwete amewataka raia hao
wapya wawe waadilifu na kufuata sheria zote za nchi

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR),
Joyce Mends-Cole (kushoto) akimuonesha Rais Jakaya Kikwete (kulia) mchoro
unaoonesha jinsi wakimbizi wa Burundi walivyoingia nchini wakati walipokuwa
wanatoka nchini kwao mwaka 1972. Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia
kwa wakimbizi 162,156 waliokuwa raia wa Burundi katika hafla iliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Tabora leo. Katikati ni Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.

Rais Jakaya Kikwete (wasita kushoto waliokaa), mabalozi na wawakilishi
wa mashirika ya kimataifa nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (watano kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi,
Harrison Mseke (watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa (wasita kulia) wakiwa katika
picha ya pamoja na sehemu ya raia wapya 162,156 wa Tanzania (nyuma waliosimama)
baada ya kupewa vyeti vya uraia na Rais Kikwete katika hafla iliyofanyika
katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini humo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
KUTOKA:KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
EmoticonEmoticon