Wanawake
wengi wanaojifungua kwa upasuaji, hukumbana na changamoto kubwa ya
kurudisha miili yao katika hali ya kawaida. Hali hii husababishwa na
muda wa kuuguza kidonda na hofu ya kujitonesha.
Wataalamu
wa afya kutoka Kituo cha Malezi na Ushauri cha Hispania (CMA) wanaeleza
kuwa ni lazima mama aliyejifungua kwa upasuaji achukue tahadhari kubwa
kabla ya kufanya mazoezi yoyote.
Awe karibu na daktari wake ili amuulize maswali kadhaa kabla ya kujichukulia uamuzi kuhusu mwili wake katika kipindi hicho.
Hata kama umbile lako lilikuwa kubwa kiasi gani kabla na baada ya ujauzito, huna budi kusubiri kwa kipindi hicho.
Kubeba
mtoto na kuzaa kunaathiri, lakini upasuaji husababisha mwili kufubaa na
kuzorota. Hiyo ni changamoto inayomlazimisha mtu kujipanga ili kurudia
hali yake aliyokuwa nayo awali.
Jambo
la msingi ni mhusika kushauriana na daktari wake kabla ya kuanza
mazoezi. Miongoni mwa mambo yatakayozingatiwa kabla ya mazoezi ni
kidonda kupona ili kisitoneshwe kwa mazoezi.
Hata hivyo, kuna mazoezi mepesi ambayo mgonjwa anaweza kujipima mwenyewe kwa kuhakikisha anauweka vyema mwili wake.
Hii ni pamoja na kufanya mazoezi ya kutembea hapa na pale kama vile kando ya uwanja pembeni mwa nyumba.
Zoezi
hili ni zuri tu kwa kukurudisha mtu katika hali ya kawaida na kumpa
hamu ya mazoezi baada ya upasuaji lakini pia ni njia nzuri ya kupata
hewa safi.
Kuna
mazoezi ya sakafuni, kupiga msamba ambayo yatasaidia kuimarisha misuli
inayozunguka maeneo ya uke na mapaja. Misuli hii ndiyo inayokuwezesha
kudhibiti mkojo.
Mazoezi
yasiyoweza kuleta maumivu kwenye viungo lakini bado yakakuweka katika
umbile zuri, kwa mfano kuogelea. Unaweza kuendesha baiskeli pia au
kukimbia.
Kama
ilivyo kwa wanawake waliojifungua kwa upasuaji, ndivyo inavyotakiwa
kuwa kwa mtu mwingine yeyote ambaye ameugua na kulazwa kwa matibabu.
Mara baada ya kupata nafuu na kuweza kutembea, anapaswa kufanya mazoezi
polepole ili kuurejesha mwili katika hali yake ya kawaida.
Akiwa anafanya mazoezi mepesi itakuwa rahisi kuendeleza mazoezi aliyokuwa anafanya awali bila kuwa na shida.
Hivyo
ni kusema mtu yoyote anapaswa kufanya mazoezi kulingana na uwezo alio
nao kwa lengo la kuuweka mwili katika hali nzuri ya kiutendaji
EmoticonEmoticon