·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA
TUHUMA ZA WIZI WILAYA YA MBOZI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NA BHANGI JIJINI MBEYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI
WA VWAWA MJINI WILAYA YA MBOZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWILE LISBON @ MANGEU (25)
ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI WALIOAMUA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUMKAMATA KWA TUHUMA ZA KUVUNJA NA KUIBA
KATIKA NYUMBA YA MTU MMOJA AITWAYE BRIGATE
SICHALWE, MKAZI WA VWAWA MJINI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 24.09.2014
MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO
MAENEO YA FLORIDA VWAWA MJINI, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA
WA MBEYA. AIDHA, TAARIFA ZA AWALI ZINADAI KUWA MAREHEMU ALIKUWA MHALIFU MZOEFU
NA ALIKUWA AKISAKWA NA POLISI KWA MUDA MREFU KUTOKANA NA KUTUHUMIWA KWA VITENDO
VYA UVUNJAJI NA KUIBA KATIKA MAENEO MBALIMBALI.
KATIKA CHUMBA
ALICHOKUWA AKIISHI MAREHEMU, KUMEPEKULIWA NA KUKUTWA MAGODORO MAWILI
YALIYOTAMBULIWA KUWA NI YA WIZI. HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA
TUKIO HILI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA – MBOZI.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHRISTOPHER GEOFREY (23) MKAZI WA MBALIZI AKIWA NA MISOKOTO
MITATU YA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAMU
15 IKIWA KWENYE GANDA LA SIGARA.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE
25.09.2014 MAJIRA YA SAA 16:30 JIONI
HUKO MAENEO YA MSITU WA KILIMO, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA
WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon