·
MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA AMEKUTWA AMEUAWA NA
MWILI WAKE KUTELEKEZWA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA AMBAYE
HAKUWEZA KUTAMBULIKA JINA WALA MAKAZI YAKE AMEKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA USONI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.09.2014
MAJIRA YA SAA 07:30 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA ILOLO, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA
MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI. KATIKA ENEO LA
TUKIO, KUMEKUTWA GODORO MOJA JIPYA, MASHUKA MAWILI NA SKETI MOJA RANGI NYEUSI.
MWILI WA
MAREHEMU UMEKUTWA NA MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWANI NA USONI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI VWAWA KWA UCHUNGUZI PAMOJA NA
KUTAMBULIWA NA NDUGU. JITIHADA ZA KUWATAFUTA WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1.
JANE ANDEMBWISYE (41) MKAZI WA
UYOLE KATI NA JACKSON MLUNGU (58) MKAZI WA ITEZI WAKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 11/2.
MSAKO HUO
UMEFANYIKA MNAMO TAREHE 11.09.2014
MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO
UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI
WAUZAJI NA WANYWAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon