OSCAR PISTORIUS ATACHOMOKA OKTOBA?


Pistorius amepewa dhamana na Jaji Masipa hadi Oktoba 13, hukumu yake itakapotolewa na yuko hatarini kufungwa miaka 15 jela kwa kuua bila kukusudia, na miaka mitano kwa matumizi mabaya ya bastola mgahawani.

Familia ya marehemu Reeva Steenkamp, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na mwanariadha mwenye ulemavu raia wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius imekasirishwa na uamuzi wa jaji wa kesi hiyo iliyotikisa dunia. 

Jaji anayeendesha kesi hiyo, Thokozile Masipa, alimfutia Pistorius hatia ya kuua kwa kukusudia, hivyo kumkuta na hatia ya mauaji ya kutokusudia, sambamba na hatia nyingine ya matumizi mabaya ya bastola akiwa mgahawani. 

Pistorius amepewa dhamana na Jaji Masipa hadi Oktoba 13 hukumu yake itakapotolewa na yuko hatarini kufungwa miaka 15 jela kwa kuua bila kukusudia, na miaka mitano kwa matumizi mabaya ya bastola mgahawani. 

Hatia hizo, zimemsukuma mama wa Reeva, June Steenkamp kusema kuwa mwanawe ambaye alikufa vibaya hakufanyiwa haki katika mfululizo wa kesi hiyo, kwa kitendo cha kumfutia mashitaka ya kuua kwa makusudi. 

June amesema kuwa, hakuamini kwamba Jaji Masipa alikubali ushahidi wa Pistorius, kwamba aliftaua risasi bafuni akidhani kuwa alivamiwa na majambazi na hakujua kuwa ni Reeva ndiye aliyekuwa ndani ya bafu ya nyumba yao. 

Hata hivyo, mjomba yake Pistorius, alimshukuru Jaji Masipa kwa kumuondolea mashtaka ya mauaji ya kukusudia mwanariadha huyo maarufu barani Afrika. 

Pistorius ataendelea kuwa nje kwa dhamana hadi Oktoba 13, hukumu yake itakapotolewa, huku familia hiyo ya Steenkamp ikiona haikutendewa haki bila kujali hukumu atakayopewa baada ya kuondolewa shitaka la kuua kwa makusudi.
Previous
Next Post »