TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 15.09.2014.
·
MTU MMOJA MKAZI WA IPINDA WILAYA YA KYELA AUAWA
KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI.
·
MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA
BARABARANI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WAHAMIAJI HARAMU SITA RAIA WA NCHI YA BURUNDI, KONGO NA ETHIOPIA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI KWA TUHUMA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUGANO JOHN (36) MKAZI WA IPINDA JUU
AMEUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA WANANCHI WALIOAMUA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI MAWE NA MARUNGU KUTOKANA
NA TUHUMA ZA WIZI WA BAISKELI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 14.09.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI
CHA LUTUSYO, KIJIJI NA KATA YA TALATALA, TARAFA YA NTEBELA, WILAYA YA KYELA,
MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKAMATWA NA WANANCHI HAO AKIWA NA
BAISKELI YA WIZI NA KISHA KUANZA KUMSHAMBULIA KWA KUMPIGA HALI ILIYOPELEKEA
KIFO CHAKE. MSAKO WA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA
WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA
ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NASIBU
LANGISON (21) MKAZI WA IGOGWE –
TUKUYU AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA KATIKA HOSPITALI YA
WILAYA RUNGWE KWA MATIBABU BAADA YA PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA KUACHA NJIA
NA KUANGUKA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 13.09.2014 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI NA
KATA YA ILIMA, TARAFA YA PAKATI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA
BARABARA YA TUKUYU/KYELA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO, ABIRIA ALIYEKUWA AMEPAKIZWA
KATIKA PIKIPIKI HIYO AITWAYE LILIAN
RAMADHAN (19) MKAZI WA BAGAMOYO
ALIPA MAJERAHA NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA RUNGWE.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA RUNGWE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU SITA AMBAO NI 1. ZINABU ASSETA (29) RAIA
NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA 2. KADEH
WAHALU (27) RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA 3. JACKQULINE UHASI (07)
RAIA NA MKAZI WA NCHINI BURUNDI NA WENGINE WALIOFAHAMIKA KWA JINA MOJA MOJA BEATHA (30) RAIA NA MKAZI WA NCHINI BURUNDI OLIVER (25) RAIA NA MKAZI WA NCHINI KONGO DEVINE (25) RAIA NA MKAZI WA NCHINI
BURUNDI.
WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.09.2014 MAJIRA YA SAA 20:50 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI NA
KATA YA MKOLA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. WAHAMIAJI
HAO WALIKAMATWA WAKIWA WANASAFIRISHWA KWENYE BASI T.791 ACJ AINA YA SCANIA MALI YA KAMPUNI YA SUPER SERVICE. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA MASHAKA
KATIKA MAENEO YAO ILI UCHUNGUZI UFANYWE DHIDI YAO NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SPELAZA
FURAHISHA (35) MKAZI WA UPENDO
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA LITA TANO [05].
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.09.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI
CHA LEGEZA, KIJIJI CHA UPENDO, KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO.
KATIKA MSAKO WA TATU, MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LAITON MTAWA (18) MKAZI WA MALANGALI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA AKIWA NA KETE 14 ZA BHANGI
SAWA NA UZITO WA GRAMU 70.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.09.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO MAENEO YA
SOKONI, KIJIJI NA KATA YA MALANGALI, TARAFA YA BULAMBYA, WILAYA YA ILEJE, MKOA
WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUTWA NA BHANGI HIYO ALIYOKUWA AMEIFICHA KWENYE MFUKO
WAKE WA SURUALI BAADA YA KUPEKULIWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
NA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
Imesainiwa
na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon