.Ni rafiki wa bi harusi ambaye alikuwa awe matroni
.Mume achanganyikiwa kwani ndiye Best man
.hekaheka zatokea ajifungulia kwenye gari
Na MOblog Team, kwa msaada wa mtandao wa Daily Mail
MWANAMKE ambaye alitakiwa kuwa matroni na kisha kumkatalia rafiki yake kwa kuwa alikuwa mjamzito na aliogopa kumharibia shughuli yake, amejikuta akikimbilia katika gari kwa ajili ya kujifungua muda mfupi tu baada ya kuingia katika sherehe za rafiki yake.
Alisema awali kwamba alikataa kuwa matroni kwa kuhofia sit u kuvuruga shughuli ya jamaa yake pia alikuwa anaona ataharibu picha za harusi.
Lakini kwa kitendo chake hicho alikuwa ndani ya harusi kw akujinafasi sana.
Imeelezwa katika mtandao kwamba akiwa kama mgeni katika sherehe hiyo mwanadada huyo alijikuta akuitoka kasiu katika sherehe za rafiki yake aliyetambulika kwa jina la Amanda Vasey baada ya kuvunja chupa wakati akiingia kushiriki sherehe hiyo.
Vasey, 37, anasema kwamba moja ya picha znuri kabisa anayioipenda ni ya yeye, mumewe Steven Vasey, 35, na marafiki zao hao Gareth na Amanda Hutchinson wakiwa hospitalini na binti wa marafiki zao baada ya kujifungua kwa dharura katika gari.
Ndoa ya Vasey, ilifanyika Jumamosi katika hoteli ya King iliyopo Darlington.
Bibi harusi Amanda Vasey akielekea wodini kumsalimia shoga yake.
“nilikuwa ndio namaliza kujivika nguo wakati Gareth, ambaye ndiye msimamizi wa mume wangu alipoingia akikimbia na kusema kwamba Amanda ameanza kazi ya kujifungua.
“kwanza sikuamini nilizania anafanya mzaha kwani alikuwa na kitetemo cha hotuba katika harusi kiasi alikuwa akitania kwamba atamwaga maji kwa kuhangaika. Sasa aliposema mkewe amevunja chupa nilidhani anatafuta njia ya kukwepa kutoa hotuba ya harusi.
“Baadae nikaona hatanii ndipo mama yangu na wasaidizi wengine wakatoka mbuio kwenda kutoa msaada.
“ walilazimika kuchukua shuka kubw akutoka katika hoteli ili kumpatia faragha ndani ya gari ambako ndilko alikuwakiwa akijifungulia.”
Anasema kulikuwa na hamaniko kubwa kiasi ya kwamba kila mtu alikuwa anataka kumuona na hivyo wakalazimika kuifunika gari ili amalize shughuli yake kwanza.
“Bahati nzuri hapakuwepo na shida na hivyoi motto aliingia duniani salama.” Alisema bi harusi.
Hutchinson alijifungua motto aliyekuwa na paundi saba na aonzi 9 na akakambizwa hospitalini akifuatiwa na mumewe Gareth, 28, hivyo kumwacha bwana harusi bila msimamizi.
Best man na maharusi wakifurahia habari njema za kujiungua salama kwa matroni kabla ya kuelekea hospitali.
Vasey amesema: ‘Amanda ni mmoja wa marafiki zangu wakubwa na nilitaka awe sehemu ya waliokaribu nami siku ya harusi yangu, lakini alipogundua kwamba yeye ni mjamzito alikataa kuwa matroni.
“Alikuwa ameshajaribu nguo za matroni na kila kitu lakini baadae akasema ataharibu picha za harusi akakataa kushiriki. NBikamwambia usijali lakini akasema hataki kuharibu picha .
“ni kitu cha kuchekesha kidogo, lakini hakutaka hata kushiriki vikao kwa sababu yeye ni mjamzito, hakutaka kuwa katika hartusi lakini mwishoni mwa siku kila kitu kilimgusa yeye.”
Bi Harusi Amanda Vasey na shoga yake Amanda Hutchinson aliyembeba mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja Alfie., huku mume wake Gareth Hutchinson (mpambe wa bwana harusi) akiwa amembeba binti ya mchanga aliyezaliwa muda mfupi kabla ya ndoa ya bwana harusi Steven Vasey (aliyesimama).
Rafiki huyo aliomba msamaha mfululizo wakati bi harusi alipoenda kumtembelea baada ya kumaliza hafla ambayo haikucheleweshwa.
Vasey alisendelea kusema: “alikuwa anaomba msamaha muda wote kwamba ameniharibia siku yangu. Kumbe sivyo kabisa ameleta Baraka kubwa katika siku nyangu ya harusi na sasa nitamkumbuka motto muda wote.
“ Nilipoenda kumtembelea tulipoonana nililia, wote tulilia, ilikuwa siku yangu kubwa. Ninaolewa na Steven na rafiki yangu anamkaribisha motto duniani.’
Mtoto wa Hutchinson hajapewa jina lakini wanakusudia kumpa jina la Amanda .
EmoticonEmoticon