
Watu zaidi ya nane kutoka nchi jirani ya Kenya wakishirikiana na watanzania ambao wanadhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za kivita wamevamia baa moja katika mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari na kuwaua watu wawili kwa kuwapiga risasi huku wakijeruhi wateja wengine watatu pamoja na kupora kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wateja hao na kukusanya mauzo yote ya baa hiyo ya New mzalendo.
Baadhi ya wananchi ambao wameshuhudia tukio hilo wamesema kuwa watu hao wamevamia baa hiyo wakiwa wamevalia nguo ambazo mara nyingi zimekuwa zikitumiwa na askari wa jeshi la polisi na kuanza kurusha ovyo risasi kisha kupora wateja walikuwa katika baa hiyo kabla ya kuingia kaunta na kupora kiasi kikubwa chafedha.
Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Tarime na Rorya kamishina msaidizi Lazaro Mambosasa, akizungumza na ITV kwa njia ya simu, amekiri kutokea kwa tukio hilo, huku akisema majambazi hayo zaidi ya manene toka nchi jirani wakishirikiana na watanzania wamefanya uhalifu huo kwa kutumia bunduki za kivita aina ya smg huku akiwataja watu walioawa kuwa Samwel Bhoke na mwingine ambaye amejulikana kwa jina moja la Leonard wote wakazi wa Sirari.
Wakati huohuo jeshi la polisi mkoani Mara limeendesha oparation kali katika wilaya zote za mkoa wa Mara na kufanikiwa kukamata nyaraka mbalimbali za serikali, madawa ya kulevya,pikipiki sita zilizokua zinatumika katika matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na bunduki moja ya kivita aina ya smg na risasi 28 katika wilaya ya Serengeti.
EmoticonEmoticon