Mtalii raia mmoja kutoka nchini Equador Amerika ya kusini amevunja rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kuupanda mlima Kilimanjaro na kushuka kwa kutumia muda wa saa sita dakika 42 na sekunde 24

Photo: Mtalii  raia  mmoja kutoka  nchini  Equador  Amerika  ya kusini  amevunja  rekodi  ya  kuwa mtu  wa  kwanza  kuupanda mlima  Kilimanjaro  na kushuka   kwa  kutumia  muda  wa  saa sita dakika  42  na sekunde  24  kupanda  na  kushuka  kwenye  mlima  huo.  Rekodi  ya  mwisho ya kupanda mlima  huo  kwa  muda  mfupi  iliwekwa mwaka 2010 na raia wa Hispania aliyetajwa kwa jina moja la Kilian  aliyetumia  saa  saba  dakika  24 . Kwa kawaida wageni wengine hupanda mlima huo kwa siku tano hadi sita.

Akizungumza  na  ITV  baada  ya kushuka  kutoka  safari hiyo  mtalii huyo  Bw. Karl  Egloff pamoja na  kuuelezea  mlima  huo  kama  kivutio cha pekee  duniani  amesema anaona  fahari  kuweka  rekodi  hiyo  aliyodai  hataisahau katika maisha yake.

Mtalii raia mmoja kutoka nchini Equador Amerika ya kusini amevunja rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kuupanda mlima Kilimanjaro na kushuka kwa kutumia muda wa saa sita dakika 42 na sekunde 24 kupanda na kushuka kwenye mlima huo. Rekodi ya mwisho ya kupanda mlima huo kwa muda mfupi iliwekwa mwaka 2010 na raia wa Hispania aliyetajwa kwa jina moja la Kilian aliyetumia saa saba dakika 24 . Kwa kawaida wageni wengine hupanda mlima huo kwa siku tano hadi sita.

 Baada ya kushuka kutoka safari hiyo mtalii huyo Bw. Karl Egloff pamoja na kuuelezea mlima huo kama kivutio cha pekee duniani amesema anaona fahari kuweka rekodi hiyo aliyodai hataisahau katika maisha yake.
Previous
Next Post »