TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 19.08.2014.
·
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA MWINGINE
KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOHUSIANISHA BASI LA ABIRIA MALI YA KAMPUNI YA
NDENJELA NA PIKIPIKI.
·
MWENDESHA PIKPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUGONGWA NA GARI LA MIZIGO MALI YA KAMPUNI YA OVERLAND.
·
MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA AMEFARIKI DUNIA
BAADA YA KUGONGANA NA PIKIPIKI NYINGINE.
·
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI NDUBATI AMEFARIKI
DUNIA BAADA YA KURUKA TOKA KWENYE GARI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
BASI LA ABIRIA
MALI YA KAMPUNI YA NDENJELA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.484 BWX AINA YA YUTONG LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA OMBENI LEOTELI KADINDA (39) MKAZI WA
SAE LILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI AITWAYE
BENARD SIMPUNGWE ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.683 CRE AINA YA T-BETTER UMRI KATI YA
MIAKA 25 – 30 MKAZI WA KIJIJI CHA
KASINDE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO NA
KWA ABIRIA WAKE AITWAYE ADELA
SAFI (09) MWANAFUNZI WA DARASA
LA PILI KATIKA SHULE YA MSINGI NYENJELE, MKAZI WA KIJIJI CHA KASINDE AMBAYE
ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA SERIKALI VWAWA.
AJALI HIYO
IMETOKEA MNAMO TAREHE 18.08.2014
MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MPUTI, KATA YA NDALAMBO, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA,
MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA TUNDUMA/SUMBAWANGA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO,
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SAFI
BENJAMINI (29) MKAZI WA KIJIJI
CHA KASINDE ALIJERUHIWA NA AMELAZWA HOSPITALINI HAPO KWA MATIBABU.
CHANZO CHA AJALI
NI MWENDO KASI WA GARI. MIILI YA MAREHEMU IMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA
NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWENDESHA
PIKIPIKI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHRISTOPHER
MAYALA (28) MKAZI WA TUNDUMA
ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.423 BBL AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA
USAJILI T. 971 CAS/T.445 CBM AINA YA
SCANIA MALI YA KAMPUNI YA OVERLAND LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA CHARLES ALOYCE (67) MKAZI WA DSM.
AJALI HIYO
IMETOKEA MNAMO TAREHE 18.08.2014
MAJIRA YA SAA 18:30 JIONI HUKO
HANSEKETWA, KATA YA IHANDA, TARAFA YA VWAWA MJINI, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA
MBEYA KATIKA BARABARA YA TUNDUMA/MBEYA. AIDHA CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO
KASI WA GARI. DEREVA AMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA WILAYA MBOZI.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWENDESHA
PIKIPIKI @ BODABODA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA STEVEN SAMWEL (20) MKAZI
WA NDAGA AKIENDESHA PIKIPIKI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI AMEFARIKI
DUNIA BAADA YA KUGONGANA NA PIKIPIKI NYINGINE AMBAYO HAIKUWEZA KUFAHAMIKA NAMBA
ZAKE ZA USAJILI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.08.2014
MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO
NDAGA, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, WATU WATANO WALIOKUWA ABIRIA KATIKA PIKIPIKI HIZO
WALIJERUHIWA 1. MOTI STEPHEN (20) MKAZI WA NDAGA 2. CHANILE AMOS 3. JULIUS SUNGURA 4. ANORD JULIUS NA 5. AMBAKISYE AMON.
MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA IGONGWE NA MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALINI
HAPO.
KATIKA TUKIO LA NNE:
MWANAFUNZI WA
SHULE YA MSINGI NDUGATI DARASA LA SABA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMBEDWILE ASANWISYE (13) AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KURUKA
TOKA KWENYE GARI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI AINA YA CANTER IKIENDESHWA
NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA KABLA HALIJASIMAMA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 17.08.2014
MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO
LUBANDA, KATA YA ILIMI, TARAFA YA PAKATI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI NI BAADA YA MAREHEMU KURUKA KUTOKA KATIKA GARI KABLA
HALIJASIMAMA NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA
WAENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA KUACHA KUPAKIZA MISHIKAKI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA USALAMA WA ABIRIA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GETRUDA KAMANGA (40) MKAZI WA MAKONGOLOSI AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA 05 PAMOJA NA MTAMBO MMOJA WA
KUTENGENEZEA POMBE HIYO HARAMU.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.08.2014
MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MAKONGOLOSI, KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA
YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MTENGENEZAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO.
AIDHA
KATIKA MSAKO MWINGINE, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRANK ISSA (22) MKAZI WA MKWAJUNI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA AKIWA NA PAKETI 15 ZA POMBE
KALI [VIROBA] AINA YA BOSS NA RIDDER.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.08.2014
MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MKWAJUNI, KATA NA TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA.
AIDHA
KATIKA MSAKO MWINGINE, ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 18.08.2014 MAJIRA YA SAA
17:00 JIONI HUKO MAENEO YA KASUMULU NA KYELA MJINI, KATA YA KYELA, TARAFA
YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LILIKAMATA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA DOUBLE
PUNCH KATONI 01, CHARGER KATONI 05, BOSS
KATONI 06, RIDDER KATONI 02 KWENYE KIVUKO CHA AMBOKIGHE NJISI WILAYANI
KYELA. WATUHUMIWA WALIKIMBIA MARA BAADA YA KUWAONA ASKARI.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA, ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA
NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI
HATARI KWA AFYA ZA WATUMIAJI.
Imesainiwa
na kutolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon