HAYA NDIYO ALIYOYAFANYA MBUNGE DAVID SILINDE JIMBONI KWAKE TANGU AINGIE MADARAKANI




 
Kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Momba Frank Mwakajoka na katikati ni Mbunge David Silinde na kulia ni Katibu mwenezi wa vijana Joseph Kayange.


Na  Saimeni  Mgalula,Mbeya

Mbunge wa Jimbo la Momba Davidi Silinde (CHADEMA), amewaeleza Wananchi wa jimbo lake maendeleo  aliyoyafanya toka alivyoingia madarakani akiwa na lengo la Wananchi kuendelee kukipenda chama cha demokrasia na maendeleo ( chadema) na kuakikisha Wanachukuwa Madaraka tena 2015.

Hayo aliyasema katika mkutano wa Hadhara ambao ulifanyika katika kituo kidogo cha mabasi Sogea katika mji mdogo wa Tunduma Uliopo jimboni hapa katika mkoa huu,alianza kwa kueleza vitu ambavyo amefanya katika jimbo hilo ni Ujenzi wa shule za msingi sita ambazo na yeye alichangia milioni 300 toka mfukoni kwake kwa ajili ya ujenzi huo mpaka kukamilika ,alisema Silinde

Pia alisema kuwa baada ya kumaliza ujenzi huo aliomba Madawati  katika Bank ya NMB  akapewa madawati 90 ambayo aligawa madawati 15 kila shule,vilevile kisima ambacho kinatoa maji yenye ujazo wa laki moja na sabini kwaajili ya usambazaji katika mji wa Tunduma,Alisema mbunge Silinde,

Aliendelea kwa kusema kuwa wamejenga Daraja ambalo ililigharimu milioni 48 kutoka Shule ya msingi Majengo Mpaka msasani watu wanapita kwa raha tofauti na zamani walikuwa wanasumbuka sana katika ufukaji alisema silinde.

Pamoja na hayo alisema kuwa alitoa milioni 16 kwakununua magodoro ambayo aliyasambaza katika vituo vyote vya Afya katika jimbo hilo,pia akijibu swali la Benard Mwashirindi ambalo aliuza hivi Utatusaidiaje Wanamomba kwa kuwa hatuna Viwanja vya michezo vya kisasa,Silinde alimjibu kwa kusema kuwa maeneo yote waliokuwa wameyatenga kwa ajili ya viwanja yote yamejengwa na watu ila kuna maeneo mengine ambyo yametengwa ambayo yapo Chapwa ila hawawezi kuanza kujenga kwasababu hawaja lipafidia za wamiliki wa viwanja hivyo alisema silinde.

Akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya viwanja hivyo alisema kuwa Halmashauli ya Wilaya ya momba imetenga shilling 404 milioni kwaajili ya kilipa fidia ndio waendeleze michezo akiwahakikishia Wananchi alisema kuwa  swala hilo lilikuwepo toka mda mrefu

Alimalizia kwa kusema kuwa maeneo hayo yametengwa kwaajili ya Ujenzi wa Halmashauli na wameshaongea na TBA pia katika maeneo hayo kunabaadhi ni kwaajili ya ujenzi wa Chuo cha ufundi,mahakama,hospitari kubwa ya Wilaya.

Previous
Next Post »