TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 16.08.2014.
·
KIKONGWE WA MIAKA 80 AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO
KICHWANI WILAYANI RUNGWE.
·
MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA
KUGONGWA NA GARI.
·
MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA
PIKIPIKI ALIYOKUWA AKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUANGUKA.
·
BWENI MOJA LA SHULE YA SEKONDARI MARANATHA
LATEKETEA KWA MOTO.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA MKAZI WA MATENKI – BODA KWA KOSA LA KUSAFIRISHA BINADAMU KINYUME CHA
SHERIA.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
KIKONGWE WA MIAKA 80
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ADAM MWANDIGA
MKAZI WA KIJIJI CHA KIBISI ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA MOHAMED MWAMELA AMBAYE ALIKUWA ANAISHI
NAYE [MTOTO WA MDOGO WA MAREHEMU].
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.08.2014 MAJIRA YA SAA
22:30 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIBISI, KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE,
WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI
WA KIFAMILIA KATI YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA.
MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI NA WATOTO WAKE WENGINE WAWILI
AMBAO HAWAKUWEPO WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA
TUKIO, JUHUDI ZA MSAKO KUMTAFUTA MTUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL
N. MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA
WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. AIDHA ANATOA WITO KWA WANAFAMILIA KUTATUA MIGOGORO YAO
YA KIFAMILIA KWA NJIA YA AMANI NA UTULIVU ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA
KUEPUKIKA.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MPANDA BAISKELI MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA TITO KIWITI (29) MKAZI WA NYENJELE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA
NA GARI LENYE NAMBA USAJILI T. 519 AEE
AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE MICHAEL KYANDO (27) MKAZI WA MAJENGO – TUNDUMA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 15.08.2014 MAJIRA YA SAA
11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA NYENJELE, KATA YA NDALAMBO, TARAFA YA
NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA SUMBAWANGA/TUNDUMA.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO CHA AFYA CHA NYENJELE. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO
KITUONI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N.
MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA
TUKIO LA TATU:
MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FAUTELI SIMFUKWE (65) MKAZI WA IYUNGA JIJI NA MKOA ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI
AMBAYO HAIKUWEZA KUFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI AMEFARIKI DUNIA BAADA YA
PIKIPIKI HIYO KUACHA NJIA KISHA KUANGUKA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO EMANUEL SIMFUKWE (27) MKAZI WA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA AMBAYE ALIKUWA ABIRIA
KWENYE PIKPIKI HIYO ALIJERUHIWA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 15.08.2014 MAJIRA YA SAA
19:30 JIONI HUKO ENEO LA MTELEMKO MSANGAMWERU, KATA YA MBALIZI, TARAFA YA
BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. MAJERUHI ALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL
N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA
TUKIO LA NNE:
BWENI MOJA LA SHULE YA SEKONDARI MARANATHA ILIYOPO
KATA YA IWINDI, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA LIMETEKETEA
KWA MOTO JANA MAJIRA YA SAA 17:20 JIONI.
MWILE
MWAMAHONJE (38) MKAZI WA MARANATHA IWINDI ALIGUNDUA KUUNGUA KWA BWENI MOJA LA
WANAFUNZI LIITWALO ‘MANDELA A’.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, MALI MBALIMBALI ZA WANAFUNZI KAMA VILE VITABU,
MAGODORO 30, VITANDA NA SEHEMU YA JUU YA PAA LILITEKETEA KWA MOTO.
CHANZO CHA MOTO HUO BADO KUFAHAMIKA. THAMANI HALISI YA
MALI ILIYOTEKETEA KWA MOTO PIA BADO HAIJAFAHAMIKA. MOTO ULIZIMWA KWA JITIHADA
ZA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI POLISI NA
WANANCHI. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL
N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI YA MAJANGA YATOKANAYO NA
MOTO KWANI YANA MADHARA MAKUBWA NA YANA SABABISHA UHARIBIFU WA MALI.
KATIKA
MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SADIKI MWANDOLUMA (30) MKAZI WA MATENKI BODA KWA KOSA LA KUSAFIRISHA BINADAMU KINYUME
CHA SHERIA.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.08.2014
MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA ENEO LA LUBELE, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA,
MKOA WA MBEYA AKIWA ANAMSAFIRISHA DESTER
TAMLATI (24) MKAZI NA RAIA WA
NCHINI ETHIOPIA KINYUME CHA SHERIA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL
N. MASAKI ANATOA WITO KWA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU
AMBAO WANAWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO,WAHAMIAJI HARAMU NA WENGINEO ILI
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa
na kutolewa na:
[BARAKAEL N.
MASAKI – ACP]
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon