Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutokomeza Ukimwi na maambukizi mapya ya Virusi hivyo vya Ukimwi kwa Watoto (AGPAHI), Laurean Bwanakunu (kulia).(Picha na Maktaba).
Na Mwandishi wetu
Watanzania wametakiwa kuepukana vitendo vya kuhamasisha ngono zembe itakayosababisha maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU).
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutokomeza Ukimwi na maambukizi mapya ya virusi hivyo vya Ukimwi kwa Watoto (AGPAHI), Laurean Bwanakunu wakati alipokuwa akitoa taarifa kuhusu ujio wa wageni kutoka nchini Marekani.
Ugeni huo utakuwa wa Rais wa EGPAF, Charles Lyons, ambye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, ambalo linajihusisha katika kusaidia kutoa huduma za kinga, matunzo na matibabu kwa watu wanaoishi na VVU.
Alisema kuzuia maambukizi mapya kwa watuwazima na watoto inawezekana bali kinachotakiwa ni kwa wananchi kubadili mitizamo yao katika kupambana na maradhi hayo.
“AGPAHI inafanya kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Tanzania katika kusaidia kutoa huduma za kinga katika baadhi ya mikoa nchin,”alisema Bwanakunu.
Aliitaja mikoa ambayo huduma za kinga, matunzo na matibabu kwa watu wanaoishi na na VVU kuwa ni Shinyanga, Simiyu na Geita.
Akizungumzia ujio wa Rais huyo, Bwanakunu, alisema utakapokua nchini utatembelea ofisi za AGPAHI, ili kufahamu maendeleo ya shirika katika uetendaji pamoja na kusalimiana na wafanyakazi wa shirika hilo.
EmoticonEmoticon