Wanafunzi wa shule ya msingi Fumbo wakalia viroba.


Asilimia 47% ya wanafunzi wa shule ya msingi Fumbo iliyopo katika kijiji cha Gereza mashariki katika kata ya Kwagunda wilayani Korogwe  wanakalia katika viloba huku wengine wakitoka na mikeka majumbani mwao kufuatia shule hiyo kuwa na upungufu mkubwa wa madawati na hivyo kusababisha kushindwa kufanya vyema katika masomo yao.
Akizungumza shuleni hapo na ITV mwalimu mkuu wa shule hiyo Bwana Benedict Mnkondo amesema mahitaji ya shule hiyo ni madawati 140 lakini yaliyopo ni 78 hatua ambayo imesababisha kuwa na upungufu wa madawati 62.
 
Bwana Mnkondo amesema changamoto hiyo ni ya muda mrefu kwa zaidi ya miaka 7 na ameshawasilisha taarifa ya maandishi kwa idara ya elimu wilaya ya Korogwe na kuahidiwa kuwa tatizo hilo watalitafutia ufumbuzi hatua ambayo imesababisha wananfunzi kukalia viloba,mikeka na mabusati.
 
Kwa upande wake mmoja kati ya wazazi waliotakiwa kueleza jitihada wanazofanya kumaliza tatizo hilo wamesema tatizo kubwa lipo kwa viongozi wao wa serikali za vijiji kwa kushindwa kuomba vibali vya kukata miti itakayowawezesha kuweka utaratibu wa kutengeneza madawati.
Previous
Next Post »