UMUHIMU WA UTUNZAJI MAZINGIRA

Saimeni na matukio Mgalula's profile photo

Na Saimeni Mgalula

Mazingira tunayoishi tumezungukwa na vitu mbalimbali vikiwemo
mito,miti ,maziwa ,Bahari na vinginevyo kwa hali hii inapaswa
kuyatunza kwa faida zetu.

Ukweli ni huu jamii ambayo hutunza mazingira huyatunza kwa kuyaweka
safi lakini kwa hapa mkoani Mbeya hususa katika mji wa Tunduma Uliopo
wilaya ya momba Mkoani hapa ,Watu wake huyatumia ovyo kwa kutupa taka
taka ovyo.

Awali Mazingira yalikuwa yanaridhisha lakini kwa sasa yamekuwa katika
hali ambayo hairidhishi kabisa.

Mazingira yamekuwa Machafu kwasababu ya ongezeko la Watu hasa katika
Maeneo ya mji ambayo huwa na wafanya biashara  mbalimbali hususa kama
wauza migahawa wakamua jusi za miwa na ukataji wa miti ovyo .

Kwa uhalisia ukataji wa miti unamadhara mbalimbali yakiwemo
mmong`onyoko wa udogo ndo maana kuna sehemu zinaitwa maporomoko .

Ukweli wa mambo uchafu wa mazingira hutokana na Gesti na mahotel
kunasababisha mazingira kuwa na muonekano mbaya ikiwa ni pamoja
uchafuzi wa mazingira hali inayoweza kusababisha watu kuugua maradhi
kama ,magonjwa ya milipuko na hata kusababisha vifo.

Na kutokuwa na mashimo Nyumbani kunatokana na kutokuwa na elimu katika
jamii hivyo ni vema wakiwemo viongozi wa Serikali za mitaa  kutoa somo juu ya
swala hilo.

Pamoja na mazingira kuwa machafu Wananchi inabidi wabadilike na wajue
jukumu la kuweka mazingira safi .

Kwa watu wanaojali afya zao na za wengine huhamasisha watu kuweka
mazingira katika hali safi lakini pia kutoa elimu juu ya madhara
yanayoweza kupatikana kutokana na uchafu wa mazingira

Hata hivyo watu au jamii kwa ujumla inatakiwa kutumia mapipa
yanayowekwa barabarani kwaajili ya kuhifadhi taka wanapaswa kuwa
makini na kuangalia vyombo hivyo kama vimejaa na kuviondoa ilikuepuka
kuzagaa pindi zitakapo tupwa kutokana na vifaa vya kuhifadhia

Aidha Serikali kwa ujumla na mabwana afya wawe makini na kudhibiti
watu ambao wanachezea mazingira wawekewe sheria kali ilikila mtu awe
anaogopa

MWISHO.
Previous
Next Post »