NOTI YA SHILINGI 500 SASA KUBADILISHWA NA KUWA SARAFU


Baada ya kuonekana noti ya shilingi 500 ina na mzunguko mkubwa wa matumizi na inachakaa kwa haraka huku kiwango chake cha kuhimili mizunguko kikiwa  ni miezi sita tu, Benki kuu ya Tanzania (BOT) inatarajia kubadili noti hiyo na kuifanya sarafu. 

Sarafu hiyo ya 500 inatarajiwa kutambulishwa na kuanza kutumika July 2014 ikienda sambamba na kipindi cha mwaka huu wa fedha ambapo sarafu ikishatoka inatarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya miaka 20 na kubaki na ubora wake uleule.
 
“Tunafanya hivi kwa sababu noti ya 500 inachakaa haraka ukulinganisha na mzunguko wake na kuwafikia watu wengi pia huchakaa haraka kutokana na mzunguko wa kushikwa na watu wanaofikia mpaka milioni moja kwa siku, hiyo ni idadi kubwa kuliko ya wanaoshika noti ya elfu 10 kwa siku," amefafanua  Afisa mkuu wa benki kitengo cha idara kurugenzi za kibenki Patrick Fata
Previous
Next Post »