TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 02.07.2014.
·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA
USONI NA MTOTO WAKE.
·
WATU WATANO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA POMBE HARMU YA MOSHI [GONGO].
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI WA NCHINI MALAWI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI KINYUME
CHA SHERIA.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MARTHA KYANDO (73) MKAZI WA KIJIJI CHA IBUNGILA AMEUAWA KWA KUPIGWA FIMBO
KICHWANI NA USONI KISHA KUNYONGWA SHINGO NA MTOTO WAKE AITWAE KISWIGO ANGANISYE (33) MKAZI WA KIJIJI CHA IBUNGILA WILAYANI RUNGWE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.07.2014 MAJIRA YA SAA
00:30 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA MPUNGUTI, KIJIJI CHA IBUNGILA, KATA YA
MALINDO, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. AIDHA INADAIWA KUWA KABLA YA KUUAWA MAREHEMU PIA ALIBAKWA.
INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO NI BAADA YA MTUHUMIWA
AMBAYE INASEMEKANA ANA MATATIZO YA AKILI KUCHUKIA BAADA YA MAREHEMU KUMPIKIA
MAGIMBI BADALA YA UGALI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
TAARIFA
ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU
WATANO KWA KOSA LA KUPATIKANA NA POMBE HARMU YA MOSHI. WATUHUMIWA HAO NI PAMOJA
NA 1. EMANUEL
SAKALA (21) MKAZI WA MWANJELWA, 2. SHABAN ZUBERI (23) MKAZI WA MWANJELWA 3.
JAMES ANDREW (24) MKAZI WA
MAKUNGULU 4. MIKIDADI MWALUGOYA (25) MKAZI WA MWANJELWA 5. SADIKI HUSSEIN (24) MKAZI WA JUAKALI.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA WAKIWA NA GONGO UJAZO WA LITA 5 KATIKA MSAKO ULIOFANYWA KATIKA
ENEO LA BENKI – MWANJELWA, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJINI MBEYA MNAMO
TAREHE 01.07.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA. WATUHUMIWA NI
WATUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA
MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU
WAWILI RAIA NA WAKAZI WA NCHINI MALAWI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
WAHAMIAJI HAO HARAMU NI PAMOJA NA 1.
THOMAS JUMA (29) NA 2. BONIFACE CHITETE
(29).
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 01.07.2014 MAJIRA YA SAA 23:15 USIKU KATIKA MSAKO
ULIOFANYIKA KATIKA ENEO LA KYELA- KATI, KATA YA KYELA-KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA
UHAMIAJI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA MASHAKA
KATIKA MAENEO YAO IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon