Wafanyakazi hawa wanataka nyongeza maradufu ya mishahara yao
Wanachama wa chama kikubwa zaidi cha wafanyakazi Nchini Afrika Kusini watagoma wakidai mshahara wao kuongezwa kwa kiwango kikubwa.
Wanachama hao wanataka mishara akuongezwa maradufu ya kiwango cha mfumo wa bei nchini humo.
Chama cha kitaifa cha wafanyakazi wa Chuma na wahandisi kinanasema kuwa zaidi ya wanachama elfu 200 watashiriki mgomo huo.
Watafanya maandamano katika miji sita muhimu nchini humo.
Mgomo huo utakua pigo kubwa katika uchumi wa Afrika Kusini ambayo imekumbwa na migomo ya wafanyikazi wa migodi na viwanda kwa miezi mitano iliyopita baada ya mgomo wa kampuni ya dhahabu nyeupe ulioisha juma lililopita
.CHANZO BBC
EmoticonEmoticon