VITUKO VYA BRAZUKA Mchezaji wa Croatia avua nguo zote mbele ya maafisa wa FIFA pamoja na waandishi wa habari


Kiungo wa timu ya taifa ya Croatia Ivan Rakitić ameonyesha kibweka mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa mzunguuko wa pili wa kundi la kwanza dhidi timu ya Cameroon, ambayo ilikubali kufungwa mabao manne kwa sifuri.
Rakitić, ameonyesha kibweka hicho baada ya kubadilishana jezi na bukta na aliyekuwa kiungo mwenzake katika klabu ya Sivilla, Stéphane Mbia wakati wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia.
Rakitic ambae amesajiliwa na FC Barcelona siku tatu zilizopita alichojoa bukta yake na kubaki na nguo ya ndani ili hali Mbia alionekana kujistiri kufuatia nguo ya kubana aliyobaki nayo mwilini.
Kitendo hicho kilifanyika mbele ya waandishi wa habari pamoja na maafisa wa shirikisho la soka duniani FIFA.
Previous
Next Post »