Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius amepandishwa tena kizimbani kujibu kesi ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya Valentine, kesi ambayo iliahirishwa wiki sita zilizopita.
Pistorius amerudishwa mahakamani kueendelea na utetezi wake baada ya kuamriwa kuhudhuria kliniki ya akili chini ya uangalizi wa wataalamu wa magonjwa ya akili baada ya mawakili wanaomtetea kudai kuwa hakuwa sawa kiakili katika usiku aliompiga risasi mpenzi wake na kumuua.
Hata hivyo katika baada ya kurudishwa mahakamani hapo, ripoti imeeleza kuwa Pistorius hakuwa na tatizo lolote la akili katika usiku huo aliomuua Reeva.
Kesi yake inaendelea na kuoneshwa moja kwa moja na BBC.
EmoticonEmoticon