TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 20.06.2014.
·
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AUAWA KWA KUPIGWA
JIWE KICHWANI.
·
MFANYABIASHARA MMOJA MKAZI WA CHANG’OMBE WAILAYANI
CHUNYA AVAMIWA NA KUPORWA VITU MBALIMBALI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI KWA TUHUMA TOFAUTI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAFUNZI WA
KIDATO CHA PILI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NZONDAHAKI ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA
JOSHUA BUKUKU (19) MKAZI WA NZOVWE AMEUAWA KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI NA MTU
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOSHUA SAID
(17) MKAZI WA SIMIKE.
INADAIWA KUWA
MNAMO TAREHE 18.06.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KATIKA UWANJA WA
SHULE YA SEKONDARI ST.MARTS ILIYOKO ENEO LA FOREST MPYA, KATA YA FOREST, TARAFA
YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA ULITOKEA UGOMVI BAINA YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA
WAKATI WAKICHEZA MPIRA WA MIGUU NA NDIPO MTUHUMIWA KUMPIGA JIWE LA KICHWANI NA
KUMJERUHI.
MHANGA ALIFARIKI
DUNIA MNAMO TAREHE 19.06.2014 MAJIRA
YA SAA 18:32 JIONI WAKATI AKIENDELEA
KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. INADAIWA KUWA MTUHUMIWA
ALIKUWA ANASOMA SHULE MOJA NA MAREHEMU NA ALIACHA MASOMO AKIWA KIDATO CHA TATU
MWAKA 2013. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MFANYABIASHARA
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA STEVEN
DAISON (33) MKAZI WA CHANG’OMBE
ALIVAMIWA AKIWA NYUMBANI KWAKE NA WATU WANNE ANAOWAFAHAMU KWA SURA NA KUMJERUHI
KWA KUMKATA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KISHA KUPORA VITU
MBALIMBALI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA
01:00 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA
MWAGALA, KIJIJI CHA CHANG’OMBE, KATA YA MBUYUNI, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA HAO WALIMJERUHI MHANGA KWA KUMKATA MAPANGA
SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KISHA KUMPORA PESA TSHS 1,800,000/=, SIMU
PAMOJA NA VOCHA ZA SIMU ZENYE THAMANI YA TSHS1,200,000/=.
INADAIWA KUWA,
KABLA YA TUKIO WATU HAO WALIFYATUA RISASI HEWANI NA GANDA MOJA LA RISASI YA
S/GUN LIMEOKOTWA ENEO LA TUKIO. MHANGA
AMEPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. MSAKO MKALI UNAENDELEA ILI KUWABAINI WATUHUMIWA
WA TUKIO HILI.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MSAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LAITON
ANYELWISYE (32) MKAZI WA KIJIJI CHA
UPENDO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.06.2014
MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI KATIKA
KIJIJI CHA UPENDO, KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA KADIL KANDAM
(22) AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA
KIBALI.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.06.2014
MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU KATIKA
ENEO LA IGAWILO, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARMU YA
MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA
MASHAKA KATIKA MAENEO YAO HASA WAHAMIAJI HARAMU ILI UPELELEZI UFANYWE DHIDI
YAO.
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon