Mume wa Flora, Emmanuel Mbasha ambaye anakabiriwa na kesi ya ubakaji amepata dhamana leo (June 19) baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama ya Wilaya ya Ilala.
June 17 bwana Emmanuel Mbasha alifika mahakamani hapo na kukana shitaka la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 anaedaiwa kuwa shemeji yake, na alipelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Muendesha mashitaka wa serikali alieleza Mahakamani hapo June 17 kuwa upelelezi wa kesi hiyho umekamilika. Emmanuel Mbasha atapanda kizimbani tena July 17 kujibu mashitaka yanayomkabili.
EmoticonEmoticon