Mataifa 31 kushiriki maonyesho Sabasaba


Mataifa 31 kushiriki maonyesho Sabasaba




MATAIFA 31 na kampuni zaidi ya 500 zimethibitisha kushiriki maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Jacqueline Maleko, alieleza hayo jijini Dar es Salaam juzi katika hafla ya kusaini mkataba wa udhamini wa mawasiliano na Kampuni ya Vodacom.
“Maonyesho haya yamekuwa kiungo kikubwa kati ya makampuni ya nje na ya ndani, na pia yanatoa nafasi kwa kampuni hizo kukutana na wateja wao na kuzungumza ana kwa ana,” alisema.
Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa washiriki ambao hawajajiandikisha kwa ajili ya mchakato wa kutafuta washindi katika makundi mbalimbali kuchukua fomu na kujiandikisha.
Pia aliwataka washiriki kujiandaa kutembelea maonyesho hayo, ili kupata fursa za masoko, uwekezaji na ajira na kusema kuwa milango itafunguliwa kuanzia Juni 28.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema ushirikiano kati yao na TanTarde umekuwa na manufaa, kwani umewezesha kujenga daraja na kutoa fursa kwa kampuni za ndani na za nje.
Previous
Next Post »