Masanja awajibu waliowashambulia yeye na Diamond kwa kutopost picha za misiba na kupost za 'batani'



Siku mbili mfululizo baadhi ya mashabiki wa sanaa Tanzania waliwashambulia Diamond Platinumz na Masanja Mkandamizaji kwa kutopost picha za misiba ya wasanii wenzao kwenye mitandao ya kijamii, huku wawili hao wakipost picha wakiwa batani huko Marekani.

“Asante Mungu North Carolina's Safe! #BadaeHudumaInaanzaa# #JumapiliMapemaaIbadaYaKwanzaWashingtonDc#.” Ilikuwa post ya mwisho ya Masanja wakati wall za wasanii wenzake zikiwa na post za picha ya marehemu George Tyson aliyefariki kwa ajali ya gari, May 30.

Baada ya kuona maelezo mengi ya mashabiki wa Instagram, Masanja alivunja ukimya na kutoa yake ya moyoni.

“Naona kuna watu wanahoji mbona siweki picha ya Misiba Inayotokea. JIBU MAISHA NI MIPANGO NA MAAMUZI NILIAMUA SITAWEKA PICHA YA MSIBA WOWOTE ISTAGRAM KWA MAANA HAISAIDII CHOCHOTE, NILIFIWA NA DADA YANGU NA MDOGO WANGU WA MWISHO NA SIJAWAHI WEKA INSTA. NACHOJUA NI KWAMBA YANAPOTOKEA HAYA NI KUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO,TENA SIO KUMSHUKURIA INSTA UNAMSHUKURU MOYONI WAKO. SO NIWAOMBE MLIOKUWA MNASUBIRI NIPOST SITAPOST NG'O!! NA KWA TAARIFA MSIBA WA ADAM NILIKUWEPO LIDAZ NA MCHANGO NIKATOA LKN SIKUWEKA PICHA ISTAGRAM. SO HUWA SIONGOZWI NA WATU KUFANYA KITU. NA NILIACHAGA BAADA YA KWENDA KWENDA KWENYE MSIBA WA NGWEA MORO NIKAWEKA PICHA RAIA WAKAANZA OOOOH UNAUZA SURA. MALA MBONA SURA HAINA MAJONZI HEE SA MNATAKA NIJIUMBE MWENYE SURA YA MAJONZI ILI NIMKOSOE MUNGU ALIYENIUMBA HANDSOME JAMANI??? NEVER SITAWEKA PICHA ZA HIVYOOO INSTA . HAPA NI MACHAPIII YA UNAITEDI MPAKA NAVYORUDI NIKAWAPE POLE WAFIWA. NADHANI KAMA ULINIFOLOOOOOO KUPATA UPDATE ZA MISIBA. U BETTER GO TO HELL ETI KIOO CHA JAMIII(kwa ku bana pua moja na kidole) KIOO CHA JAMII CHA BABAKOOO. ... #ChekilihotubaKamaLaMheshimiwaRais# #HarafuNimeliwekaKwaHerufiKubwaa# #UsichezeNaMimiKwenyeExplanesheniiiii# #HahahahaaaNaonagaCommentZaPichaZaMisibaUtasikiaSaAmewekajeKopeMsibaniAmevaajeMiwaniAmefyokofyokomsibaniYaanWaliofeliLifeWanashidaaaaa# #KumbukaNaongozwaNaRoho# #Over#”

Hata hivyo, baada ya makombora ya mashabiki hao, Diamond Platinumz aliandika post kuhusu misiba ya wasanii walipoteza maisha katika kipindi kifupi, Adamu Kuambiana, Rachael Haule na muongozaji wa filamu George Tyson.

Previous
Next Post »