Makubwa haya Mchezaji wa Kenya alipia tangazo la kumuomba mkwewe msamaha kwenye gazeti


Mapenzi yana mambo mengi, kuna waliowahi kusema mapenzi hayana baunsa wala jeshi la kupambana na hisia halisi. Kama unampenda mkeo ubaki kwako kwa njia yoyote.
Kauli hii inadhihirishwa na kitendo alichofanya mchezaji wa timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars) anaefahamika kwa jina la Francis Onyiso ambaye alikuwa matatani kuachwa na mkewe baada ya kuchepuka na mfanyakazi mwenzake halafu akakamatwa na mkewe.
Mitandao ya Kenya imeeleza kuwa bwana Onyiso alitoka usiku na mfanyakazi mwenzake na kwenda hotel fulani lakini mkewe akadokezwa na aliwafuatilia na kuwabamba.
Baada ya msala huo, inaonekana jamaa alirudi nyumbani huku akiwa ameitia doa ndoa yake na mkewe hakuonesha dalili za kumsamehe.
Katika hali isiyo ya kawaida, mwanasoka huyo aliamua kuandika ombi la msamaha na kulilipia kama tangazo likachapishwa kwenye gazeti la The Star la May 19 mwaka huu likiwa na kichwa ‘Apology’.
Msamaha huo uliochapishwa katikati ya matangazo mengine unasomeka hivi:
I Francis Onyiso, take this Opportunity to apologize to my beloved wife Janet Aoko Owino for the Pain I have caused her and the family.
I ask for forgiveness and promise never to repeat again.
Imeelezwa kuwa Francis Onyiso alilipia shilingi 2,000 za Kenya kama gharama za kuchapisha.
Previous
Next Post »