Stori kubwa inayoongelewa kuhusu tuzo hizi za BET 2014 ambazo kwenye kipengele cha tuzo inayotolewa kwa msanii/kikudi cha Afrika Diamond Platnumz pia alichaguliwa kushiriki, ni tuzo hiyo kutolewa saa kadhaa kabla ya zile tuzo za wasanii wa Marekani kutolewa…. yani kwa ufupi hafla ya utoaji wa tuzo hizi haitoi nafasi kwa tuzo ya Afrika.Kwenye exclusive interview na millard, Diamond amesema ‘tuzo ya Afrika imetolewa saa mbili asubuhi wakati tuzo za kina Chris Brown, Beyonce na wengine wakubwa zinatolewa saa kadhaa baadae usiku, Waafrika wanawekwa peke yao ila ingekua poa kama wangekua wanatoa tuzo ya Afrika palepale kama wasanii wa Marekani, ingesaidia kuunyanyua muziki wa Afrika’
Miongoni mwa waliotoa yao ya moyoni ya kutofurahishwa na utolewaji huu wa tuzo ya Afrika kivyake na kutojumuishwa na zile za wasanii wa Marekani ni msanii Ommy Dimpoz.
EmoticonEmoticon