EVANS AVEVA RAIS SIMBA


1Mgombea Urais wa Klabu ya Simba Bw. Evans Aveva akijinadi mbele ya wanachama wa klabu hiyo leo asubuhi katika uchaguzi mkuu unaofanyika leo kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es saaam, ambapo zaidi ya wapiga kura zaidi ya 2500 kutoka jijini dar es salaam na mikoa ya jirani wamejitokeza ili kupata viongozi watakaoongoa klabu hiyo kwa miaka minne mingine baada ya kikomo cha uongozi wa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Al haji Aden Rage, mpaka tunaenda hewani kazi ya kupiga kura ndiyo inaelekea ukingoni na baada ya muda mfupi ujao kazi ya kuhesabu kura itaanza rasmi uchaguzi huo unaendelea kwa amani na ulinzi umeimarishwa na jeshi la polisi, Wapiga kura wengi waliohojiwa na mndao huu wa www.fullshangweblog.com wanasema ni wazi mwelekeo wa ushindi katika nafasi ya urais unaelekea kumwendea Evans Aveva. 2Mgombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji Said Tully naye akijieleza mbele ya wapiga kura. 2aMgombea umakamu wa Rais Bw. Godfrey Nyange Kaburu naye akijieleza mbele ya wapiga kura kabla ya kuanza upigaji kura. 3Mgombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji  Asha Muhaji akiomba kura mbele ya wana Simba. 5Upigaji kura ukiendelea kwa wanachama mbalimbali. 6Katibu wa kamati ya Uchaguzi Bw. Issa Batenga akipanga mikakati ya ulinzi na wanausalama. 7Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zacharia Hanspope akizungumza na waandishi wa habari kutoka ITV wakati wa uchaguzi huo. 8Wapiga kura wakijisajiri tayari kwa kuingia kwenye ukumbi wa uchaguzi. 9Katibu wa kamati ya Uchaguzi Bw. Issa Batenga akimzuia Michael Wambura kuingia kwenye ukumbi wa mkutano kutokana na kitendo chake cha kwenda mahakamani na kuishtaki klabu ya Simba hivyo kupoteza sifa za uanamichezo wa mpira wa miguu 10Mgombea Urais Evans Aveva akiwa amekaa kabla ya kuanza kuomba kura kwa wanachama, Kushoto ni Mgombea umakamu wa Rais Jamhuri Kihwelo. 12Usajiri ukiendelea 13Mulamu Ng’ambi kulia mmmoja wa marafiki wa Friends Of Simba akiwa na wanasimba wengine kabla ya kuingia kwenye uchaguzi. 14Mgombea ujumbe wa kamati ya utendaji Bw Alfred Elia akiwa ametulia kabla ya kuingia kwenye uchaguzi huo na kuwaomba kura za ndiyo wanachama wa Simba



Previous
Next Post »