INASEMEKANA HUYU NDIO MWIZI MPUMBAVU ZAIDI DUNIANI NI KWANINI SOMA HAPA


Facebook mwiziDunia ina matukio mengi ambayo unaweza kudhani unaona maigizo lakini mwishoni utaamini unachokiona ni kitu halisi kwa kuwa hautaona majina ya wahusika yakipita hewani kama movie.
CBS Minnesota imeripoti habari ambayo inamhusisha mwizi ambaye polisi walimtaja kuwa mmoja kati ya wezi wapumbavu zaidi duniani, Nicholas Wig mwenye umri wa miaka 26.
Bwana Wig anadaiwa kuvamia nyumba ya mtu wakati mwenye nyumba hayupo na kuiba vitu kadhaa lakini mwisho akagundua kuna computer yenye internet, na ndipo alipoamua kuingia Facebook kufanya yake lakini ghafla aliondoka na kuiacha computer hiyo huku akisahau ku-log out.
Unaambiwa mwenye mali alipofika kwake alitamani kulia machozi baada ya kugundua kuwa tayari amelizwa vitu kadhaa nyumbani kwake, lakini alipoishika computer yake iliyoachwa na mwizi huyo aligundua kuwa mwizi wake aliingia Facebook na akaondoka bila ku-log out kwa hiyo taarifa zake na picha zake zote ziko wazi.
Baada ya kuripoti polisi, hatua za kumsaka zilianza mapema na wakafanikiwa kumkamata jamaa tena akiwa amevaa saa aliyoiba kwenye nyumba hiyo.
Mwanasheria wa County/wilaya ya Dakota, James Backstrom alipofanya mahojiano na SBC alitamka kuwa hajawahi kupata kesi ya mwizi mpumbavu kama ya Wig.
Previous
Next Post »