Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI imewapangia vituo vya kazi ya ualimu walimu waliohitimu Vyuo vya Ualimu Mwaka 2013 kuchukua nafasi za walimu ambao hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa kwa ajira ya Machi 2014.
Baadhi ya waombaji hawakupangiwa vituo vya kazi kutokana na kutokuwa na sifa zinazostahili kuajiriwa katika utumishi wa umma kwa mfano:- umri na maombi kutoambatanishwa na vithibitisho muhimu n.k.
Maelekezo kwa Walimu Ajira Mpya
1. Kuripoti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa kwa ajili ya kupangiwa vituo kuanzia tarehe 25/6/2014, hadi tarehe 30/6/2014.
2. Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 30/6/2014 hatapokelewa tena na nafasi yake atakuwa ameipoteza.
3. Walimu hawa ni wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi kufuatia Orodha iliyotangazwa Machi 2014 hivyo OWM – TAMISEMI haitafanya mabadiliko yeyote ya vituo katika orodha hii.
Yafuatayo ni Majina ya Walimu Wapya ( na vituo vya kazi ) waliohitimu vyuo vya Ualimu mwaka 2013
-------------------------------------------------------------------
1. Walimu wa Astashahada Bofya Hapa
2. Walimu wa Stashahada Bofya Hapa
3. Walimu wa Shahada Bofya Hapa
EmoticonEmoticon