·
MZEE WA MIAKA 70 AUAWA KWA KUMWAGIWA
MAJI YA MOTO AKIWA NYUMBANI KWAKE.
·
WATU WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI
WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA
KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA NCHINI ZAMBIA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA SILAHA
BUNDUKI AINA YA GOBOLE.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA BHANGI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MZEE
WA MIAKA 70 ALIYETAMBULIKA KWA JINA
LA FOLO MWALUSEPO MKAZI WA KIJIJI
CHA IGUNDU WILAYA YA CHUNYA ALIKUTWA AMEUAWA
KWA KUMWAGIWA MAJI YA MOTO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA NYUMBANI
KWAKE
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 06.05.2014
MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA ISOKO, KIJIJI CHA IGUNDU, KATA NA TARAFA YA KIWANJA WILAYA
YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILI KINACHUNGUZWA, JUHUDI ZA
KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
WATU
WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LUTIA
KISAMBUKA @ MWAKAPETA (40) 2.
VERONICA MTWEVE (41) NA 3. NIKUSEKELA MBOLYE (70) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ISANGE WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO
BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.599 ALH AINA YA MITSUBISHI
CANTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NDINANI MWANGOLELA KUSHINDWA KUPANDA SEHEMU
YENYE MWINUKO KUTOKANA NA UTELEZI NA KISHA KURUDI NYUMA NA KUPINDUKA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 06.05.2014
MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO
KATIKA KIJIJI CHA ISANGE, KATA YA ISANGE, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA RUNGWE,
MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA ISANGE/MBIGILI. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU
WENGINE WAWILI WALIPATA MAJERAHA, WALITIBIWA NA KURUHUSIWA. GARI HILO LILIKUWA
LIMEBEBA MZIGO WA MADUMU 100 YA MAZIWA
YENYE UJAZO WA LITA 20 PAMOJA NA MAGUNIA
10 YA MAHINDI NA VIAZI. DEREVA ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA
TUKIO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] WA
TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA NAKONDE NCHINI ZAMBIA
WAMEKAMATA SILAHA/ BUNDUKI MOJA AINA YA
GOBOLE IKIWA NA RISASI TATU [03] ZA S/GUN.
KATIKA
MSAKO HUO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 06.05.2014
MAJIRA YA SAA 06:45 ASUBUHI HUKO
ENEO LA CUSTOM-TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA,
MKOA WA MBEYA, MTUHUMIWA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA RIG MKAZI WA NAKONDE-ZAMBIA ALIKIMBIA
MARA BAADA YA KUWAONA ASKARI HAO NA
KUTUPA MFUKO ULIOKUWA NA SILAHA HIYO. AIDHA MTUHUMIWA MMOJA AITWAYE BARBARA
CHUULU MWANS (45) MWALIMU SHULE
YA SEKONDARI SINAZONGWE SOUTHERN PROVINCE ZAMBIA AMBAYE ALIKUWA NA MTUHUMIWA
ALIYEKIMBIA AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO ZAIDI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI
KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA ILI WAKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
KATIKA
MSAKO WA PILI ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 06.05.2014
MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO
KATIKA MTAA WA IGOGWE TUKUYU MJINI, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU,
WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA
MAJINA YA 1. EMANUEL GIBSON (31) MKAZI WA IGOGWE NA 2. EMANUEL HELELA (27)
MWALIMU SHULE YA SEKONDARI LUANGWA, MKAZI WA LUANGWA WAKIWA NA BHANGI MISOKOTO
KUMI [10] SAWA NA UZITO WA GRAMU 50.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KAWA
AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon