Ø
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWSHIKILIA WATU
WAWILI KWA TUHUMA ZA MAUAJ1.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO
KWA KUKUTWA NA FUNGUO BANDIA 203.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA WATU WATATU
KWA KUKUTWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] NA MTAMBO MMOJA.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATU WANNE KWA KUFANYA BIASHARA SEHEMU
ISIYORUHUSIWA.
TUKIO
LA KWANZA.
JESHI LA POLISI MKOA WA LINAWSHIKILIA
WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA MAUAJ1.
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI WA FAMILIA MOJA JERI KAPONDA [22] NA ROGER KAPONDA [19] WOTE WAKAZI WA
KIJIJI CHA ISUTO WILAYA YA MBARALI KWA
KOSA LA MAUAJI.
AWALI TAREHE 18.05.2014 MAJIRA YA SAA 22:00HRS USIKU HUKO KATIKA KIJIJI
CHA ISUTO, KATA YA CHIMALA, TARAFA YA
ILONGO, WILAYA YA MBARALI WATUHUMIWA WALIMSHAMBULIA BAHATI SANGA [40] MKAZI WA KIJIJI HICHO KWA KUMPIGA FIMBO,NGUMI NA
MATEKE TUMBONI NA KIFUANI KISHA KUMFUNGIA NDANI YA NYUMBA YAO HADI TAREHE 20.05.2014 ALIPOFANIKIWA KUTOROKA NA KWENDA KUTOA TAARIFA POLISI NA
BAADAE KULAZWA HOSPITALI YA MISHENI
CHIMALA HADI ALIPOFARIKI DUNIA TAREHE 21.05.2014
MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA WAKATI
AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU. MAREHEMU BAHATI
SANGA ALIKUWA MFANYAKAZI NYUMBANI KWA DAVID
KAPONDA [BABA WA WATUHUMIWA]
AKIFANYA KAZI ZA KILIMO,BIASHARA NA KUTUNZA MIFUGO. CHANZO CHA TUKIO NI UPOTEVU
WA PESA KIASI CHA TSHS 7,000,000/=.TARATIBU
ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA INA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE.
KATIKA
MSAKO.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 12 KUTOKANA NA MISAKO
MBALIMBALI ILIYOFANYIKA. KATIKA TUKIO LA
KWANZA JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WATANO KWA KUKUTWA NA FUNGU BANDIA 203
WALIZOKUWA WAKIZITUMIA KUFANYA UHALIFU/KUIBA KATIKA MAHOTELI MBALIMBALI JIJINI
MBEYA. WATUHUMIWA HAO NI 1. JUMA TURUKA [35], 2. BABTISTA KINUNDA [23], 3. NOEL MLELWA [20] , 4. ABDUL SALUM [36] NA 5. IDDY SADICK [26] WOTE WAKAZI WA SOWETO JIJINI MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA SAA
09:00HRS ASUBUHI KATIKA ENEO LA MABATINI JIJINI MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA
ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA
TUKIO LA PILI JESHI LA POLISI
LIMEMKAMATA JAIRO MWAKIBINGA [23] MKAZI WA MAMA JOHN AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 250.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014
MAJIRA YA SAA 15:30HRS ALASIRI HUKO KATIKA MTAA WA RUANDA NZOVWE, KATA
YA ILOMBA,TARAFA YA IYUNGA JIJINI MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA
ILIAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA
TUKIO LA TATU JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA JIJI LA MBEYA
WALIWAKAMATA WATU WANNE KWA KUFANYA BIASHARA SEHEMU ISIYORUHUSIWA. WATUHUMIWA
HAO NI 1. JOHN JACOB [25],MKAZI WA
MAJENGO, 2. KHATIBU HASSAN
[31],MKAZI WA SOKOMATOLA ,3. PENDO
CHAULA [29],MKAZI WA MAJENGO NA 4. TUMAINI
ERNEST [33] ,MKAZI WA ITIJI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA
SAA 10:00HRS HUKO ENEO LA STENDI KUU YA
MABASI KATA NA TARAFA YA SISIMBA
JIJINI MBEYA. WATUHUMIWA WALIFIKISHWA
MAHAKAMANI NA KUPATIKANA NA HATIA, WOTE WALILIPA FAINI YA TSHS 50,000/= KILA MMOJA.
AIDHA KATIKA MISAKO MINGINE ILIYOFANYIKA JESHI LA POLISI LIMEFANIKIWA KUWAKAMATA WANAWAKE WATATU 1. GRACE LUGANO [45],MKAZI
WA MAFIATI, 2. MOSHI PAUL [35] MKAZI WA
IYUNGA NA 3. ELIZA DANFORD [28],
MKAZI WA NDAYELA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA
MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 4.5
PAMOJA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA
POMBE HIYO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA
YA SAA
13:00HRS MCHANA NA SAA 18:00HRS
JIONI HUKO KATIKA MAENEO YA MAFIATI NA
IYUNGA JIJINI MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA
DAWA ZA KULEVYA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII HUSUSANI VIJANA KUKABILIANA NA
UMASIKINI KWA KUFANYA KAZI HALALI BADALA YA KUWA
NA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA KWA
KUFANYA KAZI HARAMU IKIWA NI PAMOJA NA UHALIFU KWANI HATIMA WATAKUMBANA NA MKONDO WA SHERIA NA KUKAMATWA.
Signed by:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ].
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
EmoticonEmoticon