Ø JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI
KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI KATIKA MATUKIO TOFAUTI.
Ø JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA
MTU MMOJA KWA KUKUTWA NA POMBE KALI[ VIROBA].
Ø WAHAMIAJI HARAMU 17 WAKAMATWA KWA KUINGIA
NCHINI BILA KIBALI
KATIKA
MISAKO.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA KUTOKANA NA MISAKO MBALIMBALI
ILIYOFANYIKA. KATIKA TUKIO HILO JESHI LA
POLISI LINAMSHIKILIA OSCAR S/O MBELEWA,[36],MKAZI
WA KAFUNDO- IPINDA MKAZI WA KIJIJI CHA MAZIMBO
KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI KG
72 KWENYE GUNIA AKIWA NA PIKIPIKI YAKE YENYE NO T.477 CMZ AINA YA SANLG. TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 20.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI
STAMICO, KIJIJI NA KATA YA MKOLA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
AIDHA; JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA CASIAN S/O JOSEPH, [19], MKAZI WA
UBARUKU AKIWA NA BHANGI KETE 65,
SAWA NA UZITO WA GRAM 325. TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 20.05.2014
MAJIRA YA SAA 17:00HRS KATIKA KIJIJI
NA KATA YA UBARUKU, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. TARATIBU
ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
VILEVILE; JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA HASSAN S/O ISMAIL, [30], MKAZI WA
MBUGANI AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA]
ZILIZOPIGWA MARUFUKU AINA YA BOSS KATONI MOJA [01]. TUKIO HILO LIMETOKEA
TAREHE 20.05.2014 MAJIRA YA SAA 11:25HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
LUKUYU, KATA YA MWAYA, TARAFA YA NTEMBELA, WILAYA YA KYELA,
MKOA WA MBEYA, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE
MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA BHANGI/POMBE
HARAMUZILIZOPIGWA MARUFUKU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA NYABEDA
S/O SAMSON, [32] RAIA NA MKAZI WA NCHINI BURUNDI PAMOJA NA WENZAKE 16
WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. AIDHA ALIKAMATWA MTANZANIA HAMIS S/O MWAKALINGA [29] MKAZI WA
SOWETO AKIWA ANAWASAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU HAO. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO
TAREHE 20.05.2014 MAJIRA YA SAA 01:00HRS HUKO MWANJELWA STENDI YA TUKUYU,
KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA, TARATIBU ZA KISHERIA
ZINAFANYWA ILI KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI. PAMOJA NA
KUMFISHA MAHAKAMANI MTUHUMIWA HAMISA
MWAKALINGA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII PINDI
WANAPOWAONA/KUWATILIA MASHAKA WATU WASIOWAHAMU KUTOA TAARIFA KWENYE VYOMBO
HUSIKA ILI WAKAMATWE NA KUHOJIWA.
Signed by:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ].
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
EmoticonEmoticon