TAARIFA YA JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE”TAREHE 06.05.2014.
·
MWANAMKE WA MIAKA 70 AUAWA NAWATU
WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA SHAMBANI.
·
MZEE WA MIAKA 70 AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUGONGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MESIA
SHOTI (71) MKAZI WA KIJIJI CHA
SISITILA ALIKUTWA AMEBAKWA KISHA KUUAWA KWA KUPIGWA NA VITU BUTU
SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA SHAMBANI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 05.05.2014
MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA
KIJIJI CHA SISITILA, KATA YA SISITILA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA JERAHA SEHEMU ZA KICHWANI. CHANZO CHA TUKIO HILO
BADO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA MBEYA.UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI BADO
UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MZEE
WA MIAKA 70 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA MKISU LEMBUKA MKAZI WA KAYUKI
AMEFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA
–TUKUYU WILAYA YA RUNGWE BAADA YA KUGONGWA NA
GARI LISILOFAHAMIKA.
AWALI
MNAMO TAREHE 04.05.2014 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA
KAYUKI, KATA NA TARAFA YA TUKUYU GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MZEE
HUYO NA KUMSABABISHIA MAJERAHA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMBAYE
PIA HAKUFAHAMIKA ALIKIMBIA NA GARI MARA
BAADA YA TUKIO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA
ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUTEMBEA PEMBENI MWA BARABARA NA KUVUKA
SEHEMU ZENYE VIVUKO ILI KUEPUKA AJALI .AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NEFA LETSON (30) MFANYABIASHARA, MKAZI WA LUPA-DARAJANI AKIWA NA POMBE KALI
[VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA RIDDER KATONI 12 NA BOSS KATONI 01.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 05.05.2014 MAJIRA YA SAA
15:30 ALASIRI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA LUPA –DARAJANI, KIJIJI CHA KIBAONI,
KATA YA CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBEHIZO.
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI MTUHUMIWA ZINAFANYIKA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA
KUACHA KUUZA/KUSAMBAZA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA
MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA RAIA NA
MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MHAMIAJI
HARAMU ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA KATIKA ENEO LA ITEZI, KATA YA ITEZI,
TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAFANYIKA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO
YAO ILI WAKAMATWE NA UCHUNGUZI DHIDI YAO UFANYIKE.
Imesainiwa
na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon