LIVERPOOL YATOKA NA SARE YA 3-3 NA CRYSTAL PALACE


In action: Goalscorer Joe Allen (left) tries to win the ball from Palace striker Marouane Chamakh

Kazini: Mfungaji wa bao la kwanza la Liverpool, Joe Allen (kushoto) akichuana na mshambuliaji wa Palace,  Marouane Chamakh
Amazing: Gayle celebrates with Yannick Bolasie, sparking roaring scenes at Selhurst Park
Ajabu: Gayle akishangilia na Yannick Bolasie, baada ya kuchafua hali ya hewa kwa Liverpool uwanja wa Selhurst Park
No avail: Palace keeper Julian Speroni can't stretch to stop Daniel Sturridge's goal for Liverpool's second
Manyoya tu: Kipa wa Palace, Julian Speroni akishindwa kuokoa mpira uliopigwa na Daniel Sturridge na kuifungia Liverpool bao la pili.
Iconic: Suarez celebrates match Alan Shearer and Cristiano Ronaldo's record of 31 goals in a season
Suarez akishangilia kufikia rekodi ya Alan Shearer na Cristiano Ronaldo ya mabao 31 kwa msimu mmoja
It's on: Suarez rushes back to the halfway line after netting Liverpool's third goal


NDOTO za majogoo wa jiji, klabu ya Liverpool  kufuta ukame wa miaka 24 bila kikombe zimeanza kufifia baada ya usiku huu kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya wenyeji Crystal Palace katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England.
Kwa matokeo ya mchezo huo, Liverpool wanapanda kileleni baada ya kufikisha pointi 81, huku Manchester City wenye michezo miwili mkononi wakiwa nafasi ya pili kwa pointi 80.
Majogoo wa jiji walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 18 kipindi cha kwanza kupitia kwa Joe Allen, baadaye dakika ya 53, Daniel Sturridge akifunga bao la pili, huku bao la tatu likifungwa dakika ya 55 kupitia kwa Luis Suarez.
Wakati Liverpool wakiamini watashinda mechi ya leo, kibao kilibadilika dakika ya 79 baada ya Damien Delaney kusawazisha bao la kwanza.
Ikiwa kama utani vile, dakika ya 81 Dwight Gayle aliisawazishia Palace bao la pili.
Liverpool wakazidi kuchanganyikiwa na kuona dakika haziendi. Mnamo dakika ya 88 Dwight Gayle aliandika bao la tatu na mechi kuisha kwa sare ya 3-3.
Baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa, Luis Suarez aliangua kilio kikubwa kwa kuamini kuwa kuna asilimia kubwa wameshaweka reheni mbio zao za ubingwa.
Liverpool wamebakiwa na mechi moja mkononi ambayo wakishinda watafikisha pointi 84, wakati Man city wakishinda mechi zao mbili watafikisha pointi 86 na kutwaa taji.
Kama Man City watashinda mechi moja na kufungwa moja, halafu Liverpool wakashinda mechi ya mwisho, basi majogoo hao wa jiji watafanikiwa kutwaa ubingwa.
Liverpool wanategemea muujiza wa soka kutokea.
Previous
Next Post »