Yanga Yamnasa Mshambuliaji wa Orando Pirates kutoka Afrika Kusini



Yanga kunasa kifaa kutoka Afrika Kusini












Mshambuliaji machachari wa Kimataifa wa timu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Gerry Eteso (23), ametua Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Eteso alipokelewa na viongozi wa klabu hiyo wiki iliyopita akisubiri kufanyiwa majaribio na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans Vans Der Pluijm na kumuandaa kwa ajili ya klabu yao.

Akizungumzia hilo, Eteso alisema amekuja Yanga kwasababu ni moja ya timu anazotamani achezee soka lake.
Eteso alisema yeye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ingawa alizaliwa Afrika Kusini, ambako alikuwa anaichezea Orlando Pirates.
Alisema pamoja na Ligi Kuu ya Afrika Kusini inaendelea, lakini ameamua kuja kusaka namba katika kikosi cha Yanga.

Eteso alisema kumekuwa na ubaguzi mkubwa kwa baada ya klabu za Afrika Kusini , kuwatumia wachezaji kigeni hali ambayo imemfanya aje Tanzania kutokana na mashabiki wao wanapenda mpira.

Kiungo ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), aliwahi kuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana waliochini ya miaka 20 ambacho kilishiriki michezo ya Olimpiki mwaka 2012 nchini Londoni, huku akitajwa kuwa moja ya wachezaji wenye uwezo wa aina yake anapokuwa uwanjani.
Previous
Next Post »