WATOTO WAWILI FAMILIA MOJA WAFA PAMOJA




Miili ya watoto wawili, Daniel Paul na mdogo wake, Emmanuel Paul ikitolewa eneo la tukio. Stori: Juma Kapipi, Tabora INAUMA sana! Watoto wawili wa kiume wa familia moja, Daniel Paul ( 8 ) na mdogo wake, Emmanuel Paul (3), wamepoteza maisha wakiwa pamoja baada ya kuteketea kwa moto ndani ya nyumba. Katika tukio lililojiri majira ya saa 1:00 asubuhi, maeneo ya Mtaa wa Rufita, Mwanza-Road mjini hapa baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto huku wakiwa wamelala ndani. Habari za awali zilieleza kuwa chanzo cha moto huo kilidaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme na kuisababishia familia hiyo majonzi makubwa ya misiba miwili kwa mpigo.

Kulia ni mama wa watoto Daniel Paul na mdogo wake, Emmanuel Paul akilia kwa uchungu. Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tabora, OCD, Samwel Mwampashe alithitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kuwa polisi watafanya uchunguzi ili kubaini chanzo kamili cha moto huo.
Previous
Next Post »