Na Martha Magessa-Iringa
Kutokana na Takwimu zilizotolewa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS juu ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kuonyesha Mkoa wa Jombe unaongoza kwa asilimia 14.8, Iringa asilimia 9.1 na Mbeya ni asilimia 9 ndani ya mwaka 2012-2013.
Tume hiyo imesema kuwa, maambukizi hayo yamepungua kidogo kutokana na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi hadi kufikia asilimia 60 ya maambukizi na kusababisha kuwepo mwamko mdogo wa kubadili tabia.
Aidha Tohara kwa wanaume imeweza kupunguza maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 60 na kuonyesha kuwa, ipo haja ya kutolewa Elimu zaidi juu ya Uelewa wa Ungonjawa wa Ukimwi na Utayari wa Kupima wa VVU kwa vijana.
Mratibu wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Mkoa wa Iringa Oweni Wimbo amesema kuwa, vijana waliyojitokeza kupia virusi vya Ukimwi ni asilimia 50 tu kwa takwimu ya mwaka 2012/2013 hali ambayo elimu kuhusu Ukimwi inaitaji kutolewa zaidi kwa vijana hususani katika maeneo ya vijijini.
Hata hivyo, mratibu hoyo amesema kuwa,Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Mkoani Iringa imeanza mkaka wa kufanya kampeni ya kuvunja mitandao ya Ngono kwa vijana kwa kutoa elimu ya Ukimwi pamoja na kuamasisha vijana kujitokeza kwa wingi zaidi na kupima afya zao.
EmoticonEmoticon