UPDATE KUHUSU Ajali iliyoua watu 19 jana usiku mkoani Singida wakiwemo askari wanne wa jeshi la polisi.

Watu 19 wa kijiji cha Utaho wilayani Ikungi wamepoteza maisha wakiwemo askari wanne wa jeshi la polisi, baada ya kugongwa na basi la Summry wakati wakiwa wana toa msaada wa kumpakia marehemu kwenye gari la polisi aliye gongwa na gari kubwa ambalo halikufahamika mara moja .
Basi hilo la kampuni ya Sumry hufanya safari zake kati ya Kigoma na Dar-es-salaam. Dereva wa basi hilo alikimbia mara tu na baada ya ajali hiyo na kulitekeleza basi hilo.
Mwandishi wa habari wa ITV alifika na kuwakuta wasafiri walionusurika wakiwa  katika kituo cha polisi cha Ikungi bila ya kujua hatima yao ya  safari baada ya basi lao kuwakanyaga na kuuwa watu 19
PICHA ZOTE NA :Elisante Mkumbo-Singida
Gari la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya mkoa wa singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa
Moja ya maiti ya ajali ya basi la sumry iliyo tokea katika kijiji cha Utaho Wilayani Ikungi ikisubiri kupakiwa katika gari la polisi.
Previous
Next Post »