RIDHIWANI KIKWETE ASHINDA KWA KISHINDO CHALINZE




Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura mjini Chalinze jana.

Ridhiwani Kikwete aliyekuwa mgombea ubunge uchaguzi mdogo jimbo la chalinze bagamoyo  mkoani pwani kupitia chama cha mapinduzi CCM ameibuka  kidedea kwa asilimia 86.61 katika uchaguzi huo na kuwamwaga wagombea  wengine kutoka vyama vine vya upinzani.

Matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha Ridhiwani ameongoza akifuatiwa na CHADEMA ,CUF,NRA na ASP.

Matokeo hayo yametangazwa usiku wa kuamkia leo April 7 majira ya saa nane usiku katika shule ya sekondari Chalinze na  Msimamizi wa uchaguzi huo  Bw.Samwel Salianga ambapo amesema CCM –Ridhiwani Kikwete amepata kura  20,828 sawa na  86.61%,Chadema-Mathayo Torongei amepata kura 2,544 sawa na asilimia 
10.58,CUF- Fabian Skauki  476 sawa na asilimia 1.98,NRA-Hussein
Ramadhani kura 60 asilimia 0.25 huku AFP Ramadhani Mgaya amepata
kura 186 sawa na asilimia 0.59

 Salianga amesema kati ya watu waliojiandikisha  katika daftari la kudumu la wapiga kura ni watu elfu 92,waliojitokeza  katika zoezi hilo ni watu 24,422 ambapo kura halali zilikuwa 24,047 na  kura 375 zikiharibika.

Wagombea waliokuwepo wakati wa kutangaza  matokeo katika uchaguzi huo na kusaini fomu ya kukubalina na matokea alikuwepo mgombea wa NRA na CCM pekee.

Aidha Wakizungumza baada ya kupokea matokeo hayo aliyekuwa mgombea wa  chama cha NRA pamoja na Ridhiwani Kikwete kupitia CCM,kila Mmoja  ameshukuru wananchi na kuahidi kushirikina na wananchalinze kuleta  maendeleo.
Previous
Next Post »