MTOTO WA MIAKA 2 AMUOKOA MAMAKE


Mtoto mwenye umri wa miaka miwili nchini Uingereza Riley Ward amepokea sifa kedekede kwa kuokoa maisha ya mamake kwa kupiga nambari ya simu 999 baada ya mamake kuzimia.
Wahudumu wa afya katika kituo cha kupokea simu za dharura nchini Uingereza walisema kuwa walipokea simu ya mtoto mdogo aliyewambia ''Mama amelala''
Wahudumu hao walifanikiwa kwenda nyumbani kwa mtoto huyo katika mtaa Leicestershire, na kumpa huduma ya kwanza mamake mtoto huyo na kisha kumpeleka hospitalini.
Walimfanyia upasuaji wa dharura baada ya kupatikana na damu iliyokuwa imeganda kichwani huku akivuja damu nyingine kutoka katika kizazi chake.
Sasa mtoto huyo Riley Ward amezawadiwa kwa kitendo chake cha ujasiri na wahudumu hao waliosema kuwa huyo ndiye mtoto mchanga kabisa kuwahi kupiga simu kituoni humo.
Mamake , Dana Henry, alimtaja mwanawe kama shujaa wake mdogo.
Dana mwenye umri wa miaka 27 alisema kuwa alishtushwa sana na kitendo cha mtoto wake aliyekuwa na uwezo wa kupiga simu.
Pia alisema kuwa ameweza kuwafundisha watoto wake wadogo namna ya kupiga simu ya dharura ikiwa yeye na mumewe hawahisi vizuri.

Chanzo BBC Swahili
Previous
Next Post »