Mhubiri mtata wa kiisilamu nchini Kenya Abubakar Shariff anayejulikana kwa jina maarufu Makaburi ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana mjini Mombasa. Polisi wamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema aliuawa na akiwa mtu mwingine aliyefahamika kama Bahero.
Makaburi aliuawa nje ya gereza la Shomi la Tewa mjini Mombasa. Marehemu Shariff alikuwa anafikishwa mahakamani mara kwa mara kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya kigaidi. Habari zinasema hali ya tahadhari imeanza kushuhudiwa Mombasa ambapo vijana wameanza kujikusanya kwa ajili ya kufanya vurugu.
Kuuawa kwa Makaburi kumetokea miaka miwili baada ya mshirika wake Aboud Rogo kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa akimpeleka mkewe hospitali mjini Mombasa, tukio ambalo lilisababisha maandamano ya siku tatu mjini humo.
EmoticonEmoticon