HIZI NDIO SIFA ZA MJASIRIA MALI SOMA ZITZKUSAIDIA KAMA UNATAKA KUBADILISHA MAISHA YAKO

Watu wengi wamekuwa wakilitumia hili jina MJASIRIAMALI bila wao kutambua kama wanalitumia sahihi au sio sahihi wengi wanaamini kuwa ni wajasiriamali lkn sio wajasiriamali ni wafanyabiashara japo wengi hujiita wajasiriamali.Mjasiriamali ni mtu gani?
Huyu ni mtu ambae anaweza kutumia jamii 
inayomzunguka ktk kuanzisha fursa mbalimbali za kibiashara ambazo zitampatia kipato,mtu huyu huweza kuitumia rasilimali watu ili kujinufaisha,watu wengi wanaamini kufungua duka ni kuwa mjasiriamali hapana unaweza kufungua duka lkn bado ulichokifungua na jamii inayokuzunguka hakina faida na ni idadi ndogo tu ya watu ndio watakubaliana nacho lkn pia umefunnua duka lkn unasubiria wateja waje tu,huu sio ujasiriamali bali ni ufanyabiashara.mjasiriamali biashara yake haina msimu maalumu lkn mfanyabiashara biashara yake inamsimu maalum.
SIFA ZA MJASIRIAMALI
1. ANAPENDA KUJIFUNZA
Hahahahaa hapa ndipo ugonjwa wa watu wengi ulipo mtu anajiita mjasiriamali lkn muulize kasoma vitabu vingapi vya ujasiriamali au kahudhuria semina ngapi za ujasiriamali watanzania wengi tunapenda sana vitu vya urahisi hatupendi kujifunza kama kweli unataka kuwa mjasiriamali au ni mjasiriamali lazima uwe na sifa hii upende kujifunza kutoka kwa watu wengine na uhudhurie semina au mafunzo mengi ya ujasiriamali lassiivyo utabaki kuwa mfanyabiashara.
2. MBUNIFU 
Mjasiriamali yoyote ni mbunifu,ninapozungumzia ubunifu  ninamaana je unapata kitu tofauti kila siku ambacho jamii yako itapendezwa nacho au umeng'ang'ania aina moja siku zote? lazima kama mjasiriamali uwe mbunifu kila siku kuhakikisha unapata njia mpya ambazo zitakufanya upanue soko lako.au kazi yako ni kuona mwenzako kafungua boutique na ww unaenda kufungua boutique
3.MTU MWENYEKUTAMBUA SEHEM YA KUPATA USHAURI
Hapa ndio watu weengi wanafeeli kwenyebiashara,anahitaji kuwa mjasiriamali au ni mjasiriamli lkn anapoenda kuomba ushauri ni kwa mtu ambae hata hajui ujasiriamali au kafanya kashindwa we unafikiri unaenda kumuomba mtu ushauri alieshindwa atakupa jibu gani? atakwambia huwezi matokeo yake na we unashindwa.
4.MTU MWNYE MAHUSIANO NA WATU MBALIMBALI YA KIBIASHARA
Watu wengi hawaamini ktk nguvu ya mtandao (power of network) kama kweli we ni mjasiriamali lazima uwe na mahusiano mazuri na watu wengi ya kibiashara lkn ukiangalia wajasiriamali wengi leo hii hawana mahusiano mazuri na watu wengine kibiashara hutaweza kukua kibiashara kama hutaweza jifunza kutoka kwa wangine jifunze kutoka kwa wengine rafiki na hutawezajifunza kama hutakuwa na mahusiano mazuri na watu wengi kibiasha.
5.ANAEPENDA USHINDANI
Siku zote kama mjasiriamali usipend kukwepa ushindani shindana ili product yako iwe bora,watu wengi hushindwa kufanikiwa ktk biashara kwasababu ya kuogopa ushindani,anashindwa kufanyabiashara fulani kwasababu washindani wengi,unapokutana na washindani wengi ndio unafaham mapungufu yako na yao ukijirekebisha unafanya product yako kuwa bora.
6.AISIEOGOPA KUSHINDWA NA KUKATA TAMAA
Watu wengi hushindwa ktk biashara kwa kuogopa kushindwa anataka kuanzisha kitu lkn cha kwanza anawaza nikifirisikka je watu siwatanicheka? acha mawazo mgando rafiki kama kweli we ni mjasiriamali au unataka kuwa mjasiriamali kamwe usiogope kushindwa kwani ninasema mjasriamali ni mtu ambae yuko tayari kushindwa na kujaribu tena (risk taker) matajiri wote unaowaona duniani wamefeli mara nyingi na ndio wakaja kufanikiwa sasa kama unataka kuwa mjasiriamali usiogope kushindwa na wala usikate tamaa ukishindwa unaanza tena na tena na tena hiyo ndio sifa ya mjasiriamali.
7.MTU ANATUMIA MUDA WAKE WA ZIADA KUFANYA KITU CHA ZIADA 
Siku zote mjasiriamali ni mtu ambaye anauwezo wa kufanyabiashara zaidi ya moja yuko tayali kutumia muda wak wa ziada kufanya kitu ambacho japo kimuingizie hata elfu kumi kwa siku mtu ambaye anauwezo wa kutumia muda wake wa ziada kufanya kitu cha ziada huwa anafanikiwa saana maana huwa hapotezi muda.
Acha kuzubaa rafiki maisha yamebadilika unatumiaje muda wako wa ziada wakati vipo vitu ambavyo unaweza fanya na kujiongezea kipato,usisubiri kesho anza leo.tumia muda wako wa ziada kuigiza kipato cha ziada.
8.ANEITUMIA JAMII INAYOMZUNGUKA KUINGIZA KIPATO
Watu wengi hushindwa kulitambua hili na kujiita wajasiriamali lkn hawajui jinsi ya kuwatumia watu wanaokuzunguka ktk kukuingizia kipato,rafiki unawatumiaje watu ambao mmekutana kwenye kikao cha harusi,kikao cha kitchen part au kikao cha familia au kwenye kahawa ktk kuitambulisha biashara yako au unajua kazi kupiga umbea tu na kulalamika biashara yako haitoki,unategemea wateja unawapata wapi kama sio hao.
Previous
Next Post »