REBECCA MALOPE AJA TAMASHA LA PASAKA




Rebecca-Malope






























MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa msanii huyo amepata kura nyingi kutoka kwa mashabiki waliompendekeza.
 
“Tunashukuru kwamba baada ya mapendekezo ya mashabiki tuliwasiliana na Rebecca ambaye ameonesha uungwana wa hali ya juu na kutukubalia ombi letu.
 
“Lakini pamoja na kukubali ana ratiba ya maonesho sehemu nyingine huko kwao, hivyo ametuambia hatatumbuiza katika mikoa yote ambayo tamasha litafanyika mwaka huu, hivyo tutaangalia wapi tumpangie kulingana na ratiba yake.
“Lakini
niwahakikishie mashabiki wetu kwamba msanii huyo tutakuwa naye na sasa ni suala la Kamati ya Maandalizi kuona ratiba yake ilivyo na kisha nasi tumuweke kwenye ratiba yetu ili mashabiki wafurahi,” alisema Msama.

Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).
Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambao tayari wameshathibitisha ni Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro, Rose Muhando na kwaya ya Kwetu Pazuri wote wa Tanzania.
Previous
Next Post »