NINI MAONI YA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KUHUSU MUUNDO WA SERIKALI TATU SOMA HAPA



"Mfumo huu (Serikali tatu) nao kwa sasa unaonekana bado hautaondoa manung'uniko kwa upande wa Zanzibar

a) Mfumo wa Shirikisho la Serikali Tatu utatoa mamlaka ya ndani kwa nchi mbili zinazounda
Muungano huu na kuwa na Serikali zake za kusimamia mamlaka hayo lakini bado mamlaka ya kidola (sovereignty) yatabaki katika Serikali ya Muungano. Madai makubwa yanayotolewa na Zanzibar hivi sasa yanahusu kurejesha 'sovereignity' ili kuifanya Zanzibar, serikali yake na viongozi wake wawe na hadhi ya kutambuliwa kitaifa na kimataifa. Hilo halitapatikana katika mfumo wa Serikali tatu.

c) Upo uwezekano wa kuendelea kuwepo kwa kutoaminiana kutokana na kila nchi kuwa na Serikali yake na hivyo kuwa na chombo cha kupanga mambo yake, hali inayoweza kuifanya Serikali ya Muungano ijikute haina uwezo wa kuzisimamia Serikali hizo za mamlaka ya ndani na hivyo kupoteza uhalali wake kisiasa.

Zanzibar na mustakabali wa Muungano (1964-2013)

Maoni binafsi ya Maalim Seif Sharif Hamad
Previous
Next Post »